13. Kutafuta kinga kwa asiyekuwa Allaah ni katika shirki

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا

”Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa watu wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia mzigo.” (al-Jinn 72:06)

2- Khawlah bint Hakiym (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Yeyote atakayetua mahali na akasema:

أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ الله التامَّاتِ من شَرِّ مَا خَلَقَ

“Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia dhidi ya maovu Aliyoyaumba.”

hakitomdhuru kitu mpaka atapoondoka mahali hapo.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Bi maana kitendo hichi ni shirki kubwa kama mfano wa ´ibaadah zengine anazofanyiwa asiyekuwa Allaah. Kwa sababu kuomba ulinzi ni ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ

“Na pindi utakapokuchochea uchochezi kutokana na shaytwaan basi mtake kinga Allaah.” (al-A´raaf 07:200)

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ

”Sema: “Najikinga na Mola wa watu.” (an-Naas 114:01)

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ

”Sema: “Najikinga na Mola wa mapambazuko.” (al-Falaq 113:01)

Kuhusu kuomba ulinzi kutoka kwa viumbe waliohai, mbele yako na wenye uwezo, hakuna neno. Kama ambavyo mtu anaomba kutokamana na mtumwa wa mtu au mtoto wake. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ

“Akamsaidia yule ambaye katika kundi lake dhidi ya yule ambaye ni katika adui wake.” (al-Qaswasw 28:15)

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا

”Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa watu wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia mzigo.”

Aayah hii iliteremshwa juu ya watu ambao walikuwa wakiwaomba ulinzi wale viongozi wa majini. Hivo ndivyo walivyokuwa waarabu katika kipindi cha kikafiri. Wanapotua sehemu basi wanasema:

“Tunamuomba ulinzi kiongozi wa bonde hili kutokamana na wale wapumbavu katika watu wake.”

Kitendo hichi ni katika matendo ya watu wa kipindi cha kikafiri. Ni wajibu kumtekelezea hayo yote Allaah pekee. Allaah amesema:

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

فَزَادُوهُمْ رَهَقًا

“… basi wakawazidishia mzigo.”

Bi maana majini waliwazidishia watu uwoga zaidi. Watu watu walipowaogopa majini basi majini yalizidi kuwa na kiburi. Kuna baadhi ya Salaf wamesema kinyume na hivyo kwamba watu waliwazidishia majini kiburi na jeuri. Maana zote mbili ni za sawa. Pindi mwanadamu anapowaomba majini ulinzi basi huingiwa na majivuno na jeuri na huku mwanadamu anaingiwa na woga zaidi kuwaogopa majini. Allaah amewataja katika mazingira ya kuwakaripia, kwa hiyo ina maana kwamba ni wajibu kuachana na kitendo hicho.

2- Khawlah bint Hakiym (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Yeyote atakayetua mahali na akasema:

أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ الله التامَّاتِ من شَرِّ مَا خَلَقَ

“Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia dhidi ya maovu Aliyoyaumba.”

hakitomdhuru kitu mpaka atapoondoka mahali hapo.”

Ameipokea Muslim.

Imependekezwa kusoma du´aa hii wakati mtu anapotua mahali fulani. Hadiyth inaonyesha fadhilah za du´aa hii ya kinga na kwamba inachangia kumlinda mtu na shari ya majini na watu. Kadhalika mtu anatakiwa kusema wakati anapoingia ndani ya ndege, anapokaa kwenye gari, anapoingia ndani ya treni na mfano wake. Imekuja katika Hadiyth kwamba imependekezwa kuisoma mara tatu. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anaomba kitu basi anaomba mara tatu.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema “maneno”. Maana yake ni kwamba maneno ya Allaah yenye kutekelezeka na ya kilimwengu ambayo hayawezi kurudishwa na chochote. Wapo baadhi ya Salaf waliosema “maneno” maana yake ni yale maneno ya Allaah ya Kishari´ah na ya Qur-aan kwa sababu ni maneno makubwa na matukufu zaidi na ni maneno ya Allaah. Tafsiri zote hizi ni haki na zote ni sifa za Allaah (Subhaanah). Maneno Yake ya kilimwengu ni yenye kutekelezeka na maneno Yake ya Kishari´ah ndio maneno bora zaidi.

Katika Hadiyth hii kuna kufanya Tawassul kwa sifa za Allaah. Salaf wameitumia Hadiyth hii kama dalili kuthibitisha kwamba maneno ya Allaah hayakuumbwa kwa sababu haijuzu kuomba kinga kwa asiyekuwa Allaah. Hadiyth inathibitisha kwamba maneno ya Allaah ni sifa miongoni mwa sifa Zake, inafaa kutaka ulinzi kwayo na kwamba hayakuumbwa.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema “hakitomdhuru kitu”. Neno “kitu” imetajwa katika mazingira ya kuenea na inahusiana na kila kitu. Hii inaonyesha fadhilah za du´aa hii na kwamba inatakikana kuitendea kazi. Kuhusu kuomba ulinzi kwa asiyekuwa Allaah na kwa sifa zake, haijuzu kwa maafikiano. Kwa sababu ni shirki.

[1] Muslim (2708).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 52-53
  • Imechapishwa: 02/10/2018