Sunnah ni kukata swawm kwa tende tosa, asipopata, basi kwa tende za kawaida, asipopata, basi kwa maji. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifuturu kwa tende tosa kabla ya kuswali. Isipokuwa tende tosa basi tende za kawaida. Isipokuwa tende za kawaida basi glasi ya maji.”

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy[1].

Asipopata tende tosa, tende za kawaida wala maji basi akate swawm kwa kile kitachomkuia chepesi katika chakula na kinywaji.

[1] Ahmad (12612), Abu Daawuud (2356) na at-Tirmidhiy (695).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/380)
  • Imechapishwa: 03/04/2021