Kichwa cha khabari hichi, na kadhalika kichwa cha khabari “Sayyid Qutwub yaquul bi Khalq-il-Qur-aan”[1] kulitokea kisa cha ajabu na cha kuchekesha pindi nilipokutana na Shaykh Bakr al-Madiynah nikiwa pamoja na mtoto wangu Ahmad na nafikiri kuwa na yeye alikuwa pamoja na mtoto wake mkubwa. Tukaanza kuzungumzia juu ya kichwa cha khabari na kitabu. Shaykh akadai kuwa nimemdhulumu Sayyid Qutwub. Wakati wa mjadala akakiri kuwa hajasoma isipokuwa sehemu yake tu. Nikamwambia tusome mlango uliyobaki ambapo nimetoa mifano miwili kuonyesha namna ambavyo Sayyid Qutwub anavyojuzisha kwa asiyekuwa Allaah kuweka Shari´ah. Hakusoma mifano miwili hiyo. Iko namna hii:

“Hakuna neno iwapo mtu ataweka hukumu ya kimataifa inayotokomeza utumwa.”

Haya yamesemwa na Sayyid mara nyingi katika “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan”.

Mfano wa pili ujamaa wake uliyopindukia:

“Nchi ina haki ya kupora mali na utajiri wote na kuigawa upya. Mambo ni namna hii hata kama mali hii ilisimamishwa na kukuzwa katika njia inayokubaliwa na Uislamu.”

Akakataa kusoma milango miwili hii na akataka kitabu kisimamishwe kwa kuwa na hasira kwa Sayyid Qutwub. Hakujali kabisa yaliyofanywa na Sayyid Qutwub juu ya haki ya Allaah, Uislamu, Maswahabah na juu ya Ummah. Nilipoona msimamo huu wenye utata na wenye kushtua, nikamwambia:

“Wewe una nafasi ya juu katika mahakama. Inafaa kuhukumu kitabu changu namna hiyo baada tu ya kusoma kipande kadhaa kutoka kwenye milango miwili?”

Akaanza kucheka na hakuweza kujibu. Badala yake akaendelea na hukumu yake ya batili.

[1] Sayyid Qutwub anasema kuwa Qur-aan imeumbwa.