13 – Da´wah isiyokuwa na matunda yenye kutaka tu kuwakusanya watu

Napenda kuwakumbusha ndugu zangu wote na kina dada wenye kusoma makala hii na kadhalika waislamu wengine wote watazame mvi zangu na umri wangu mkubwa wote huu na wakati huo huo niliishi na muasisi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun Hasan al-Bannaa. Alikuwa akiita makundi na mapote yote ya Kiislamu katika umoja na wakati huo huo kila mmoja aendelee kushikamana na kubaki kuwa Suufiy, Shiy´iy, Mu´taziliy, Sunniy…

Ahl-us-Sunnah wengi wakamshauri na khaswa Shaykh Muhammad Haamid al-Faqiy (Rahimahu Allaah), muasisi wa Answaar-us-Sunnah. Hasan al-Bannaa alimtembelea nyumbani kwake. Shaykh Muhammad Haamid akamwambia kuwa mkusanyiko huu hauwezi kufanikiwa ikiwa kama haupitiki chini ya ´Aqiydah ya Tawhiyd ambayo Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wameshikamana nayo. Amesema hivo kutokana na umbali mkubwa kati ya mapote haya katika misingi.

Pamoja na hivyo Da´wah hii ambayo lengo lake kubwa ni kutaka tu kuwakusanya watu haikupata natija yoyote.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Bannaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 37-38
  • mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy