Sa´iyd bin ´Aamir adh-Dhwuba´iy, mwanachuoni wa Baswrah, amesema:
”´Aqiydah ni mbaya zaidi kuliko ya mayahudi na manaswara. Mayahudi, manaswara na watu wa dini zingine wamekubaliana na waislamu ya kwamba Allaah (´Azza wa Jall) amelingana juu ya ´Arshi, lakini wao wanasema ya kwamba juu ya ´Arshi hakuna chochote.”
Ameipokea Ibn Abiy Haatim.
´Abbaad bin al-´Awaam amesema:
”Nilizungumza na Bishr al-Mariysiy na wafuasi wake na kuona kuwa mwisho wa maneno yao wanachotaka kusema ni kwamba hakuna yeyote juu ya mbingu. Naona kuwa wasiozeshwe na wala wasirithiwe.”
Ameipokea al-Bukhaariy katika ”Khalqu Af´aal-il-´Ibaad” na Ibn Abiy Haatim katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”.
al-Asma´iy amesema:
“Mke wa Jahm alifika wakati bwana mmoja alipomwambia kuwa Allaah yuko juu ya ´Arshi. Ndipo akasema: “Aliyefupika juu ya kilichofupika?” al-Asma´iy akasema: “Mwanamke huyu amekufuru kutokana na matamshi haya.”
Ameipokea Ibn Abiy Haatim katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”.
Muhammad bin Musw´ab amesema:
“Yeyote anayesema eti Wewe huongei wala kuonekana Aakhirah, basi ni mwenye kukanusha uso Wako. Nashuhudia ya kwamba uko juu ya ´Arshi, juu ya mbingu saba, si kama wanavyosema maadui Zako mazanadiki.”
Ameipokea ´Abdullaah bin Ahmad na ad-Daaraqutwniy.
Haajib at-Twusiy amesema: Muhammad bin Hammaad ametuhadithia: Nimemsikia Wahb bin Jariyr akisema:
”Jihadharini na maoni ya Jahm. Hakika wao walikuwa wanajadiliana nami ya kuwa hakuna mungu yeyote juu ya mbingu. Hakika hapana vyengine hayo ni katika wahy wa Ibliys, hayo si chochote isipokuwa ni ukafiri.”[1]
Imaam ash-Shaafi´iy amesema:
“´Aqiydah ambayo mimi niko juu yake na ambayo nimewaona maswahibah zangu, Ahl-ul-Hadiyth kama vile Sufyaan na Malaik, ni kukiri ya kwamba hapana mungu wa haki mwingine isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah… na kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake juu ya mbingu Zake. Anawakaribia viumbe Vyake Anavyotaka na anashuka kwenye mbingu ya chini Anavyotaka …”[2]
Ameipokea Shaykh-ul-Islaam al-Hakaariy na ´Abdul-Ghaniy al-Maqdisiy na wengineo.
ar-Rabiy´ amesema:
”Nimemsikia ash-Shaafi’iy akisimulia Hadiyth kisha bwana mmoja akamwambia: “Je, unaiamini, ee Abu ´Abdillaah?” Ndipo akajibu: “Ikiwa nitasimulia Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha nisiifanyie kazi, basi nakushuhudisheni ya kwamba akili yangu imepotea.”[3]
Ibn Abiy Haatim amesema: Yuunus bin ´Abdil-A´laa ametuhadithia: Nimemsikia Abu ´Abdillaah Muhammad bin Idriys ash-Shaafi´iy (Radhiya Allaahu ´anh) akisema wakati alipoulizwa kuhusu sifa za Allaah na nini anachoamini:
“Allaah (Ta´ala) anayo majina na sifa zilizotajwa ndani ya Kitabu Chake na ambazo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewasimulia nazo ummah wake. Hakuna yeyote ambaye imemthubutikia hoja anapaswa kuzikanusha. Ikiwa mtu atazikataa baada ya hoja kuthibitika kwake, basi ni kafiri. Ama kabla ya kuthibitika hoja, anapewa udhuru kutokana na ujinga wake, kwa sababu maarifa haya hayawezi kufikiwa kwa akili, tafakuri au fikira. Lazima azithibitishe sifa hizi na kuzikanushia kufanana na viumbe, kama ambavyo Yeye Mwenyewe amejikanushia nazo:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[4]
Ukhaliyfah wa Abu Bakr ni sahihi. Allaah alihukumu hivo juu ya mbingu Zake na zikakusanyika nyoyo za Maswahabah wa Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya hilo.
[1] Swahiyh kwa mujibu wa Ibn-ul-Qayyim katika “Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”, uk. 85, ambaye amesema kwamba ”Haafidhw Muhammad bin ´Uthmaan ameisahihisha katika kijitabu chake cha ´Aqiydah.”
[2] Cheni ya wapokezi ni dhaifu kwa mujibu wa adh-Dhahabiy katika “al-´Uluww”, uk. 120.
[3] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibuwa al-Albaaniy katika “Swifatu Swalaat-in-Nabiy”, uk. 44-47.
[4] 42:11
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 57-60
- Imechapishwa: 23/12/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 57-60
Imechapishwa: 23/12/2025
https://firqatunnajia.com/13-basi-nakuwa-nimeondokwa-na-akili/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket