Download

25 – ´Abdullaah bin Idriys (afk. 192), mmoja katika wanazuoni wakubwa.

Abu Haatim ar-Raaziy amesema: al-Hasan bin as-Swabbaah ametuhadithia:

”´Abdullaah bin Idriys aliulizwa: ”Tuko na watu wanaosema kuwa Qur-aan ni kiumbe.” Akauliza: ”Je, ni katika manaswara?” Kukasemwa: ”Hapana.” Akauliza: ”Je, ni katika mayahudi?” Kukasemwa: ”Hapana.” Akauliza: ”Je, ni katika waabudia moto?” Kukasemwa: ”Hapana.” Akauliza: ”Ni kina nani sasa?” Kukasemwa: ”Ni katika waislamu.” Ndipo akasema: ”Sio katika waislamu.” Kisha akasema:

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Allaah hawezi kuwa Mwenye kuumbwa. Mwingi wa rehema hawezi kuwa Mwenye kuumbwa. Mwenye kurehemu hawezi kuwa Mwenye kuumbwa. Hawa ni mazandiki.”[1]

Kumepokelewa mfano wa hayo kutoka kwa Imaam Ibn Idriys al-Awdiy kwa cheni nyingine ya wapokezi. Alikuwa hana kifani katika zama zake na mwenye shani kubwa.

[1] Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Kuna masimulizi mengine mfano wa hayo ambayo mtunzi wa kitabu ameyaashiria. Ameyapokea ´Abdullaah bin Ahmad katika “as-Sunnah”, uk. 8: Ahmad bin Ibraahiym ametuhadithia: Yahyaa bin Yuusuf az-Zimmiy ametuhadithia:

”Wakati tulipokuwa kwa ´Abdullaah bin Idriys alijiliwa na bwana mmoja akasema: ”Ee Abu Muhammad, unasemaje juu ya mwenye kudai kuwa Qur-aan ni kiumbe?” Akauliza: ”Je, ni katika mayahudi?” Akajibu: ”Hapana.” Akauliza: ”Je, ni katika manaswara?” Akajibu: ”Hapana.” Akauliza: ”Je, ni katika waabudia moto?” Akajibu: ”Hapana.” Akauliza: ”Ni kina nani sasa?” Akajibu: ”Wapwekeshaji.” Akasema: ”Sio katika wapwekeshaji; ni mazanadiki. Yeyote anayedai kuwa Qur-aan imeumbwa anadai kuwa Allaah ameumbwa. Allaah anasema:

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.” (01:01)

Allaah hawezi kuwa Mwenye kuumbwa. Mwingi wa rehema hawezi kuwa Mwenye kuumbwa. Mwenye kurehemu hawezi kuwa Mwenye kuumbwa. Huo ndio msingi wa uzandiki. Allaah amlaani yule mwenye kusema hivo. Usiketi nao na wala usioe kwao.”

Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Wanaume wake ni wanaume wa Swahiyh. Ahmad bin Ibraahiym ni yule ad-Dawraqiy mwenye kuhifadhi. al-Bukhaariy amemfanyia ufuatiliaji katika “Khalqu Af´aal-il-´Ibaad”, uk. 69, kupiita kwa Abu Ja´far Muhammad bin ´Abdillaah.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 152
  • Imechapishwa: 22/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

Turn on/off menu