Haya ndio makundi yaliyotajwa na mtunzi wa kitabu kisha akasema:

“Na mfano wao kama vile Ash´ariyyah ambao ni wafuasi wa al-Hasan bin Ismaa´iyl ash-Ash´ariy. Alikuwa mwanzoni mwa jambo lake akilimi katika madhehebu ya Mu´tazilah mpaka alipofikisha umri wa miaka arobaini kisha akatangaza kutubu kwake kutokamana na jambo hilo na akabainisha upotofu wa madhehebu ya Mu´tazilah na akashikamana na madhehebu ya Ahl-us-Sunnah – Allaah amrehemu. Kuhusu wale wanaojinasibisha naye walibakia katika madhehebu maalum yanayotambulika kama madhehebu ya Ashaa´irah. Hakuna wanachothibitisha katika sifa za Allaah isipokuwa saba peke yake hali ya kudai kuwa akili ndio imezifahamisha. Zilizosalia zote wanazipindisha maana. Zimetajwa katika shairi hili:

1 – Uhai.

2 – Mjuzi.

3 – Muweza.

4 – Mwenye kuzungumza.

5 – Matakwa.

6 – Usikizi.

7 – Uoni.

Wana Bid´ah nyinginezo kuhusu maana ya maneno, uwezo na mengineyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 163
  • Imechapishwa: 22/02/2023