128. Watu wenye ´Aqiydah ya Mu´tazilah hii leo

Hata hivyo miongoni mwa mambo yanayosikitisha sana ni kwamba wengi katika wafuasi wake, na khaswa wale waliokuja nyuma, wameyakengeusha maneno yake haya kwa njia yenye kukataliwa, kwa sababu wameyafanya kuonekana kuwa anazungumzia maneno ya kinafsi. Mchukue Shaykh al-Kawthariy – mbebaji wa bendera ya kizazi cha waliokuja nyuma na mwenye kuwatusi Salaf – kama mfano wakati anayawekea maelezo majadiliano ya Abu Yuusuf na Abu Haniyfah na kusema, baada ya kutaja maono mbalimbali kuhusu maneno ya Allaah (Ta´ala) na kuwakejeli Ahl-ul-Hadiyth kuwa wapuuzi na hawana maana yoyote kwa sababu tu wanasema kuwa maneno ya Allaah ni kwa herufi na sauti:

”Kwa hivyo makinzano yamebaki kati yetu sisi na Mu´tazilah. Ni jambo ambalo kimsingi linarejea kuthibitisha au kukanusha maneno ya nafsi na iwapo Qur-aan ni maneno au nyenzo hii (bi maana yenye kusikika) ambayo inatokana na herufi. Mosi ni kuwa tunaafikiana juu ya kuzuka kwa nyenzo yenye kuzuka na umilele wa maneno ya kinafsi endapo jambo hilo limethibiti. Kutokana na utafiti wa mazungumzo ya nafsi na kwamba Qur-aan ni ile aina inayopaswa kufasiriwa ule mjadala uliokuweko baina ya Abu Haniyfah na Abu Yuusuf ulioendelea kwa miezi sita, ambapo hatimaye wakakubaliana kusema kwamba yule mwenye kusema kuwa Qur-aan ni kiumbe ni kafiri.”

Namna hii ndivo al-Kawthariy alivoenda sambamba na Mu´tazilah katika kupinga ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Lakini yeye na wale watu mfano wake, wanaojidhihirisha kuwa eti ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, amefanya hivo kwa njia ya ujanjaujanja. Hata hivyo yale yanayofichwa na vifua vyao ndio makubwa na mabaya zaidi. Wanatetea maneno ya ndani ya nafsi yasiyosikika. Wanapoulizwa ni nani ambaye alianza kuzungumza kwa Qur-aan na ni nani ambaye ameisikia kutoka kwake, hawajui wajibu nini. Uhakika wa mambo ni kwamba ´Aqiydah inayokanusha maneno ya Allaah (Ta´ala) inarejea kwamba Qur-aan sio maneno ya Allaah. Mambo yakishakuwa hivo ni kwamba haina maana kwamba iwapo wa kwanza kuzungumza kwa Qur-aan ni Jibriyl au Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam). Hakika maneno yao yanakutana na yale maneno yaliyosemwa na makafiri wa Quraysh ambao Allaah amewanukuu kwamba wamesema kuhusu Qur-aan.

إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ

“Hii si chochote isipokuwa ni maneno ya mtu!”[1]

Ijapo hawasemi waziwazi kama wao ya kwamba Qur-aan ”hakika hapana vyengine ni maneno ya mtu”, kwa hali yoyote wanasema kuwa ni maneno ya Jibriyl au maneno ya kiumbe mwingine. Hatimaye wanaafikiana kusema kwamba Qur-aan sio maneno ya Allaah (Ta´ala). Allaah ndiye mwenye kutakwa msaada dhidi ya upotofu huu ambao wameingia ndani yake vizazi vingi vilivyokuja baadaye. Hivo ndivo Allaah (Ta´ala) anavyowaadhibu wale wanaopinda kutokana na mfumo wa Salaf na Ahl-ul-Hadiyth – Allaah atukutanishe nao na atufishe juu ya ´Aqiydah yao! Kwa ajili hiyo Wakiy´ bin al-Jarraah amesema:

”Usizungumze kwa ´Aqiydah yao kwamba Qur-aan ni kiumbe. Kwani hiyo ni ´Aqiydah yao mbovu kabisa. Ajenda yao pekee ni ukanushaji.”[2]

 Halafu al-Bayhaqiy akasema baada yake:

”Tumesimulia mfano wa haya kutoka kwa wanazuoni wengi ulimwenguni – Allaah awaridhie! Kutokana na ninavyojua hakujasihi kutoka kwa yeyote kutoka katika zama za Maswahabah na wanafunzi wao ambaye alionelea kinyume na hivo – Allaah awe radhi nao wote!”

[1] 74:25

[2] Khalqu Af´aal-il-´Ibaad, s. 71, na al-Bayhaqiy katika  ”al-Asmaa’ was-Swifaat”, uk. 254.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 156-157
  • Imechapishwa: 22/07/2024