Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Endapo mtu atasema kuwa kama Allaah angelikuwa juu ya ´Arshi basi ingelipelekea akawa Ndiye mkubwa, mdogo zaidi au mwenye kulingana na ´Arshi na yote hayo hayawezekani kabisa, basi anatakiwa kujua kuwa hakufahamu uwepo wa Allaah juu ya ´Arshi isipokuwa kile anachofahamu kutoka katika viwiliwili vilivyoumbwa. Malazimsiho haya yanatokana na uelewa huu. Kuhusu kulingana juu ambako kunaendana na utukufu wa Allaahna ni maalum Kwake, basi hakupelekei kitu katika malazimisho haya ya batili.
MAELEZO
Mu´attwilah wanasema Allaah amelingana juu ya ´Arshi – na ´Arshi ni kiumbe – basi aidha Allaah ni sawa na ´Arshi kwa ukubwa, ni mkubwa kuliko ´Arshi au ni mdogo kuliko ´Arshi – Allaah ametukuka kutokana na wanayosema! Kwa sababu maneno haya hayamstahikii Allaah. Haya yanahusika kwa viumbe tu. Kiumbe kinapokuwa juu ya kiumbe kingine, hakikosi kuwa ama sawa nacho, kikubwa kuliko hicho au kidogo kuliko hicho. Ama Muumba, hili halilazimiki katika haki Yake kwa sababu ya tofauti iliyopo kati ya Muumba na kiumbe. Kisha haya ni mazungumzo kuhusu namna, jambo ambalo hatuna ujuzi nalo.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 215
- Imechapishwa: 10/07/2026
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Endapo mtu atasema kuwa kama Allaah angelikuwa juu ya ´Arshi basi ingelipelekea akawa Ndiye mkubwa, mdogo zaidi au mwenye kulingana na ´Arshi na yote hayo hayawezekani kabisa, basi anatakiwa kujua kuwa hakufahamu uwepo wa Allaah juu ya ´Arshi isipokuwa kile anachofahamu kutoka katika viwiliwili vilivyoumbwa. Malazimsiho haya yanatokana na uelewa huu. Kuhusu kulingana juu ambako kunaendana na utukufu wa Allaahna ni maalum Kwake, basi hakupelekei kitu katika malazimisho haya ya batili.
MAELEZO
Mu´attwilah wanasema Allaah amelingana juu ya ´Arshi – na ´Arshi ni kiumbe – basi aidha Allaah ni sawa na ´Arshi kwa ukubwa, ni mkubwa kuliko ´Arshi au ni mdogo kuliko ´Arshi – Allaah ametukuka kutokana na wanayosema! Kwa sababu maneno haya hayamstahikii Allaah. Haya yanahusika kwa viumbe tu. Kiumbe kinapokuwa juu ya kiumbe kingine, hakikosi kuwa ama sawa nacho, kikubwa kuliko hicho au kidogo kuliko hicho. Ama Muumba, hili halilazimiki katika haki Yake kwa sababu ya tofauti iliyopo kati ya Muumba na kiumbe. Kisha haya ni mazungumzo kuhusu namna, jambo ambalo hatuna ujuzi nalo.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 215
Imechapishwa: 10/07/2026
https://firqatunnajia.com/128-ndio-maana-fikira-za-muattwilah-zikawa-batili-2/