Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kila mmoja anayekanusa na kufananisha ametumbukia katika kukanusha na kufananisha. Wale wanaokanusha hawafahamu sifa za Allaah isipokuwa tu kwa ile njia ianyolingana na viumbe. Kutokana na ufahamu huo ndipo wakaendelea na kukanusha majina ya Allaah. Kwa msemo mwingine ni kwamba wamekufanya kati ya kukanusha na kufananisha; wameanza kufananisha kwanza, kisha baadaye ndipo wakakanusha. Kushabihisha na kufananisha kwao huku kunatokana na kwamba wamefahamu majina na sifa za Allaah kwa inayolingana na majina na sifa za viumbe. Halafu ndipo wakamkanushia Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yale majina na sifa zinazolingana Naye (Subhaanahu wa Ta´ala).
MAELEZO
Uhakika wa mambo ni kwamba wakanushaji ni wafananishaji kwa sababu wamekusanya kati ya kukanusha na kufananisha. Kwani hawakuelewa katika sifa za Allaah isipokuwa yale yanayofanana kwa sifa za viumbe. Ndiyo maana wakazikanusha kwa hoja ya kutakasa. Hivyo wao kwanza walifananisha, kisha pili wakakanusha.
Wafananishaji pia ni hivyo hivyo walifananisha kwanza, kisha wakakanusha pili, kwa kuwa walimkanushia Allaah ukamilifu Wake na wakamsifu kwa upungufu na wakasema kuwa sifa Zake ni kama sifa za viumbe. Kwa hiyo wafananishaji walikanusha ukamilifu wa Allaah na wakanushaji walikanusha majina na sifa ambapo wakazipinga. Hivyo makundi yote mawili ni wakanushaji na wafananishaji.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 214-215
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kila mmoja anayekanusa na kufananisha ametumbukia katika kukanusha na kufananisha. Wale wanaokanusha hawafahamu sifa za Allaah isipokuwa tu kwa ile njia ianyolingana na viumbe. Kutokana na ufahamu huo ndipo wakaendelea na kukanusha majina ya Allaah. Kwa msemo mwingine ni kwamba wamekufanya kati ya kukanusha na kufananisha; wameanza kufananisha kwanza, kisha baadaye ndipo wakakanusha. Kushabihisha na kufananisha kwao huku kunatokana na kwamba wamefahamu majina na sifa za Allaah kwa inayolingana na majina na sifa za viumbe. Halafu ndipo wakamkanushia Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yale majina na sifa zinazolingana Naye (Subhaanahu wa Ta´ala).
MAELEZO
Uhakika wa mambo ni kwamba wakanushaji ni wafananishaji kwa sababu wamekusanya kati ya kukanusha na kufananisha. Kwani hawakuelewa katika sifa za Allaah isipokuwa yale yanayofanana kwa sifa za viumbe. Ndiyo maana wakazikanusha kwa hoja ya kutakasa. Hivyo wao kwanza walifananisha, kisha pili wakakanusha.
Wafananishaji pia ni hivyo hivyo walifananisha kwanza, kisha wakakanusha pili, kwa kuwa walimkanushia Allaah ukamilifu Wake na wakamsifu kwa upungufu na wakasema kuwa sifa Zake ni kama sifa za viumbe. Kwa hiyo wafananishaji walikanusha ukamilifu wa Allaah na wakanushaji walikanusha majina na sifa ambapo wakazipinga. Hivyo makundi yote mawili ni wakanushaji na wafananishaji.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 214-215
https://firqatunnajia.com/127-namna-hii-wakanushaji-ni-wafananishaji-na-wafananishaji-ni-wakanushaji/