127. Hivi ndivo anatakiwa kudhaniwa Abu Haniyfah

Kuhusu yale aliyopokea al-Khatwiyb kupitia kwa Sa´iyd bin Muslim al-Baahiliy, ambaye amesema:

”Tulimuuliza Abu Yuusuf: ”Ni kwa nini hutusimulii kutoka kwa Abu Haniyfah?” Akasema: ”Unamtakia nini? Amekufa akiwa ni mwenye kusema kuwa Qur-aan ni kiumbe.”[1]

Kuthibiti maneno haya kwa Abu Yuusuf kunatakiwa kuangaliwa vyema, kwa sababu al-Baahiliy huyu hatambuliki kusimulia. Kwa sababu ameachwa na hakufanyiwa wasifu katika vitabu vya wanazuoni.  Hata Ibn Abiy Haatim hakumtaja katika kitabu chake ”al-Jarh wat-Ta´diyl”, licha ya ubobeaji na uzungukaji wake. Pengine sababu ya hayo ni yale aliyoashiria al-Khatwiyb mwishoni mwa wasifu wake:

”Asili yake anatokea Baswrah na alikuwa akiishi Khuraasaan. Mtawala alimpa baadhi ya ajira Marw. Alipofika Baghdaad akazisimulia huko. Amesimulia. Amepokea kutoka kwa mtaalamu wa lugha Muhammad bin Ziyaad al-A´rabiy. Ni kweli kwamba alikuwa bingwa wa Hadiyth na kiarabu, ingawa hakuwa mwenye kuwafunza watu.”[2]

Hata hivyo kuna mapokezi kadhaa katika ”Taariykh Baghdaad” yanayosema kuwa Abu Haniyfah alikuwa anaona kuwa Qur-aan imeumbwa. Ingawa nimekagua kwa umakini mkubwa jambo hilo na kuona kuwa cheni zake za wapokezi hazikosi kasoro, na pengine yaliyosalia yako namna hiyo. Haya khaswa kwa kuzingatia kwamba al-Khatwiyb amepokea kuwa Imaam Ahmad amesema:

”Haikusihi kwetu ya kwamba Abu Haniyfah alikuwa akisema kuwa Qur-aan ni kiumbe.”

Hivo ndivo anavyodhaniwa Imaam Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) na elimu yake. Na ikiwa hayo yatasihi kutoka kwake, basi pengine aliyasema hayo kabla ya yeye kujadiliana na Abu Yuusuf kwa miezi sita. Hatimaye akaafikiana naye ya kuwa Qur-aan sio kiumbe na kwamba mwenye kudai kuwa ni kiumbe basi ni kafiri. Uhakika wa mambo ni kwamba hii ni moja katika dalili nyingi juu ya fadhilah za Abu Haniyfah. Hakufanya kiburi wala jeuri kufuata maoni ya mwanafunzi wake Abu Yuusuf wakati ilipombainikia kuwa haki iko upande wake. Allaah amrehemu na amridhie!

[1] Taariykh Baghdaad (13/379).

[2] Taariykh Baghdaad (9/74).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 156
  • Imechapishwa: 21/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy