119 – Kuhusu kusoma Qur-aan wakati wa kuyatembelea makaburi ni jambo ambalo halina msingi wowote katika Sunnah. Bali Hadiyth zilizotajwa katika suala lililotangulia zinaashiria kutowekwa jambo hilo katika Shari´ah, kwani mambo yangelikuwa hivo basi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angelifanya na angewafundisha Maswahabah zake, khaswa kwa kuwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) – ambaye ni miongoni mwa watu anaowapenda zaidi – alimuuliza ni nini aseme anapotembelea makaburi, basi akamfundisha salamu na du´aa. Kwa msemo mwingine hakumfundisha asome al-Faatihah au Suurah nyingine katika Qur-aan. Kwa hivyo lau kusoma Qur-aan kungekuwa kumewekwa katika Shari´ah basi asingemficha jambo hilo. Kuchelewesha ubainifu wakati wa haja ni jambo lisilojuzu, kama lilivyothibiti katika elimu ya misingi. Tusemeje kuhusu kuficha?
Lau angelifundisha lolote kuhusu hilo, basi lingelitufikia.
Kwa kuwa halikupokewa kwa cheni iliyothibiti basi ikajulisha ya kuwa halikutokea.
Miongoni mwa mambo yanayotilia nguvu kutowekwa jambo hilo katika Shari´ah ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Msiyafanye nyumba zenu kuwa makaburi, kwani shaytwaan hukimbia kutoka kwenye nyumba ambayo ndani yake kunasomwa Suurah al-Baqarah.”
Ameipokea Muslim (2/188), at-Tirmidhiy (4/42) ambaye ameisahihisha, na Ahmad (2/284, 337, 378, 388) kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah. Kuna nyingine inayoitia nguvu kutoka katika Hadiyth ya as-Swalswaal bin ad-Dalahmas.
Ameipokea al-Bayhaqiy katika ”ash-Shu‘b” kama ilivyo katika ”al-Jaamiy‘ as-Swaghiyr”.
Ameashiria (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba makaburi si mahali pa kusomea Qur-aan Kishari´ah. Kwa ajili hiyo akahimiza kusoma Qur-aan ndani ya nyumba na akapiga marufuku kuzifanya kuwa kama makaburi ambayo ndani yake hakusomwi Qu-aan, kama alivyoashiria katika Hadiyth nyingine kuwa makaburi si mahali pa kuswalia pia, nayo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Swalini ndani ya nyumba zenu wala msizifanye kuwa makaburi.”
Ameipokea Muslim (2/187) na wengineo kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Kwa al-Bukhaariy kuna Hadiyth mfano wa hiyo ambaye ameiwekea mlango unaosema “Mlango unaozungumzia machukizo ya kuswali kwenye makaburi”. Akaashiria kuwa Hadiyth ya Ibn ´Umar inathibitisha kuchukia kuswali kwenye makaburi. Basi vivyo hivyo Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) inaashiria machukizo ya kusoma Qur-aan makaburini na hakuna tofauti[1]. Kwa sababu hiyo madhehebu ya wengi katika Salaf, kama Abu Haniyfah, Maalik na wengineo wanaona kuwa inachukiza kusoma Qur-aan kwenye makaburi, nao ni msimamo wa Imaam Ahmad.
Abu Daawuud amesema katika ”Masaa-il” yake, uk. 158:
“Nimemsikia Ahmad akiulizwa kuhusu kusoma Qur-aan kwenye kaburi ambapo akajibu: ”Hapana.”
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amenukuu kutoka kwao katika ”Iqtidhwaa’-us-Swiraatw al-Mustaqiym Mukhaalafati Aswhaab-il-Jahiym”, uk. 128:
“Haijulikani kutoka kwa ash-Shaafi‘iy mwenyewe maneno yoyote katika suala hili, kwani jambo hilo kwake lilikuwa ni Bid‘ah. Maalik amesema: ”Sikumjua mtu yeyote anayefanya hivyo. Basi imejulikana kwamba Maswahabah na wanafunzi wao hawakuwa wakilifanya.”
Amesema tena katika ”al-Ikhtiyaaraat al-‘Amaliyyah”, uk. 53:
“Kisomo cha Qur-aan kwa maiti baada ya kufa kwake ni Bid‘ah, tofauti na kumsomea mtu ambaye anataka kukata roho ambapo inapendekeza kumsomea Yaa Siyn.”
Lakini Hadiyth ya kusoma Yaa Siyn ni dhaifu, kama ilivyotangulia, uk. 11. Kupendekezwa ni hukumu ya Kishari‘ah na hivyo hakuthibiti kwa Hadiyth ambayo ni dhaifu, kama inavyojulikana kutokana na maneno ya Ibn Taymiyyah mwenyewe katika baadhi ya vitabu vyake na vinginevyo.
[1] Jopo la wanazuoni wameitumia kama hoja Hadiyth hii kama alivyofanya al-Bukhaariy, jambo ambalo limeungwa mkono na Haafidhw katika maelezo yake. Nimeshaeleza maneno yake katika suala lijalo, na. 128, kipengele cha 7.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 241-243
- Imechapishwa: 06/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 241-243
Imechapishwa: 06/08/2026
https://firqatunnajia.com/127-bidah-ya-kusoma-qur-aan-makaburini/