124. Mwanzo wake ni asali na mwisho wake ni sumu

Tabaka inayofuatia

18 – Jariyr adh-Dhwabiy (afk. 117-188), mwanachuoni wa Marw katika Hadiyth:

149 – Yahyaa bin al-Mughiyrah amesimulia kuwa amemsikia Jariyr bin ´Abdil-Hamiyd akisema:

”Maneno ya Jahmiyyah mwanzo wake ni asali na mwisho wake ni sumu. Wanachojaribu ni wao kusema kwamba juu ya mbingu hakuna mungu yeyote.”[1]

Yamekwishatangulia mfano wa hayo kutoka kwa Hammaad bin Zayd.

19 – Shaykh-ul-Islaam ´Abdullaah bin al-Mubaarak (afk. 118-181).

150 – Imesihi kwamba ´Aliy bin al-Hasan bin Shaqiyq amesema:

”Nilimuuliza ´Abdullaah bin al-Mubaarak: ”Ni vipi tutamtambua Mola wetu (´Azza wa Jall)?” Akasema: ”Kwamba Yuko juu ya mbingu ya saba, juu ya ´Arshi Yake. Hatusemi kama wanavosema Jahmiyyah, kwamba Yuko hapa ardhini.”

Hayo yakasemwa kuambiwa Ahmad bin Hanbal, ambapo akasema:

”Hivo ndivo tunasema.”[2]

Imekuja katika upokezi mwingine:

”Nilimuuliza ´Abdullaah bin al-Mubaarak: ”Ni vipi tunatakiwa kumtambua Mola wetu (´Azza wa Jall)?” Akasema: ”Kwamba Yuko juu ya mbingu ya saba, juu ya ´Arshi Yake. Hatusemi kama wanavosema Jahmiyyah, kwamba Yuko hapa ardhini.”

Aflah bin Muhammad amesema:

”Nilisema kumwambia Ibn-ul-Mubaarak: ”Ee Abu ´Abdir-Rahmaan! Mimi nachukia kuzungumzia sifa za Mola.” Akasema: ”Hakuna ambaye anachukia zaidi kuliko mimi, lakini wakati Qur-aan inapotamka jambo basi tunalisema na wakati masimulizi yanapokuja na jambo tunalipokea.”[3]

´Abdullaah bin Ahmad amepokea katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” kwamba bwana mmoja alimwambia Ibn-ul-Mubaarak:

”Ee Abu ´Abdir-Rahmaan! Nimekuwa ni mwenye kuogopa mbele ya Allaah (´Azza wa Jall) kutokana na wingi wa du´aa nilizoziomba dhidi ya Jahmiyyah.” Akasema: ”Usiogope. Kwani hakika wao wanadai kuwa Mola wako ambaye yuko juu ya mbingu si chochote.”[4]

[1] Mtunzi amesema: Abu Haaruun Muhammad bin Khaalid ametuhadithia: Yahyaa bin al-Mughiyrah ametuhadithia. Cheni ya wapokezi ni nzuri. Yahyaa bin al-Mughiyrah ni mkweli. Vivyo hivyo kuhusu Abu Haaruun, kama ilivyo katika “al-Jarh wat-Ta´diyl (3/2/245).

[2] Twabaqaat-ul-Hanaabilah (2/233).

[3] Simtambui ni nani Aflah bin Muhammad. Masimulizi haya yamepokelewa na al-Laalakaa’iy (1/97/2) na al-Bayhaqiy, kama ilivyo katika “al-Hamawiyyah”  ambapo Ibn Taymiyyah amesema:

”Alichokusudia Ibn-ul-Mubaarak ni kwamba tunachukia kumweleza kutokana na matashi yetu bila ya dalili na masimulizi.”

[4] as-Sunnah, uk. 07, kutoka kwa Ahmad bin Naswr bin Maalik: Bwana mmoja alinikhabarisha kutoka kwa Ibn-ul-Mubaarak. Wasimulizi wote ni madhubuti isipokuwa bwana ambaye hakutajwa jina.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 149-150
  • Imechapishwa: 21/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy