3 – Khawaarij. Nao ni wale ambao walitoka kwa ajili ya kumpiga vita ´Aliy bin Abiy Twaalib kwa sababu ya hukumu. Madhehebu yao ni kujitenga mbali na ´Uthmaan na ´Aliy na kuwafanyia uasi viongozi pale wanapoenda kinyume na Sunnah. Vilevile wanaona kuwa mtenda dhambi kubwa ni kafiri na kwamba atadumishwa Motoni milele. Wako mapote mengi.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 162
- Imechapishwa: 21/02/2023