122. Msimamo wa kati na kati baina ya kuchupa mipaka na kuzembea

Murji-ah ni kinyume kabisa na Khawaarij. Khawaarij wamechupa mipaka ilihali Murji-ah wamezembea na wakasema kuwa maasi hayadhuru kitu. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wako kati kwa kati. ´Aqiydah yao imejengeka juu ya Qur-aan na Sunnah na iko kati na kati na inaoanisha dalili. Khawaarij na Mu´tazilah wamechukua dalili za makemeo na matishio na wakaacha dalili zinazozungumzia msamaha, ama Murji-ah wao wamechukua dalili zinazozungumzia msamaha na wakaacha dalili za makemeo na matishio. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wameoanisha kati ya dalili za makemeo na matishio na dalili za msamaha. Hivo ndivo inatakiwa kufanya:

وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ

“Ama wale waliobobea katika elimu husema: “Tumeziamini; zote ni kutoka kwa Mola wetu”, na hawakumbuki isipokuwa wale wenye akili.”[1]

Wanazirudisha dalili hizi juu ya zingine. Hawachukui sehemu na wakaacha sehemu nyingine kama wanavofanya wapotofu:

فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ

“Ama wale ambao nyoyoni mwao mna upotevu hutafuta zile zisizokuwa wazi kwa lengo la kutaka fitina na kutaka kuzipotosha. Hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah.”[2]

Wapotofu wanashikamana na yale maandiko yasiyokuwa wazi na wanaacha yale maandiko yaliyo wazi ambayo yanafasiri yale maandiko yasiyokuwa wazi.

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tunawaita wale wanaoswali kuelekea Qiblah kuwa ni ”waislamu” na ”waumini”.”

Hayatakiwi kufahamika namna hii moja kwa moja. Kwa sababu watu hawa wanaweza kuwa na mapungufu katika Uislamu na katika imani yao na wakati huohuo wakaingia chini ya matishio ya Allaah (´Azza wa Jall).

[1]3:7

[2]3:7

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 132
  • Imechapishwa: 12/11/2024