3 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewapa ruhusa wanawake kuyatembelea makaburi katika Hadiyth mbili zilizohifadhiwa kwetu na Mama wa waumini; ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):
1 – ´Abdullaah bin Abiy Mulaykah ameeleza:
”‘Aaishah alikuja siku moja akitokea makaburini. Nikamuuliza: “Ee Mama wa waumini, unatokea wapi?” Akasema: “Kutoka kwenye kaburi la ‘Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakr.” Nikamwambia: “Je Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakukataza kuyatembelea makaburi?” Akasema: “Ndio, lakini kisha akaamrisha kuyatembelea.”
Katika riwaya nyingine kutoka kwake:
”Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliruhusu kuyatembelea makaburi.”
Ameipokea al-Haakim (1/376), na kutoka kwake al-Bayhaqiy (4/78) kupitia njia ya Baswtwaam bin Muslim kutoka kwa Abu at-Tayyaah Yaziyd bin Humayd, kutoka kwa ‘Abdullaah bin Abiy Mulaykah. Riwaya ya pili ni ya Ibn Maajah (1/475). al-Haakim hakusema lolote juu yake. adh-Dhahabiy amesema: “Ni Swahiyh.” al-Buuswayriy amesema katika ”az-Zawaaid” (1/988):
“Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh na wanaume wake ni wenye kuaminika.” Mambo ni kama alivosema.
Haafidhw al-‘Iraaqiy amesema katika ”Takhriyj-ul-Ihyaa´” (4/418):
”Ameipokea Ibn Abiyd-Dunyaa katika ”al-Qubuur” na al-Haakim kwa cheni ya wapokezi nzuri.”
2 – Muhammad bin Qays bin Mukh’ramah bin al-Muttwalib amesema siku moja: “Je nikusimulieni kuhusu mimi na mama yangu?” Tukadhani anamaanisha mama yake mzazi. Akasema: “‘Aaishah amesema: ”Je, nikusimulieni kuhusu mimi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?” Tukasema: “Ndio.” Akasema:
”Wakati ilikuwa ni usiku wangu ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa kwangu, aligeuka akaweka joho lake, akavua viatu vyake, akavihifadhi karibu na miguu yake, kisha akalaza upindo wa kikoi chake kitandani, akaingia kitandani. Hakukaa muda mrefu mpaka nilipoona kana kwamba amelala. Akachukua joho lake kwa upole, akavaa viatu kwa upole, akafungua mlango [kwa upole], akatoka, kisha akaurudisha [kwa upole]. Nami nikachukua ngao yangu nikajifunika kichwani, nikajifunika vizuri, nikamfuata mpaka akafika Baqiy’. Akasimama muda mrefu, kisha akainua mikono yake mara tatu. Kisha akageuka nami nikageuka, akaenda kwa haraka nami nikafanya hivyo. Akakimbia, nami nikakimbia. Akakaza mwendo, nami nikafanya hivyo. Nikamzidi mwendo na nikafika nyumbani kabla yake. Mara nikajilaza, akaja naye akaingia. Akasema: “Ni nini hiki, ee ‘Aaish, umekuwa na pumzi ya haraka?” Nikasema: “Hakuna kitu [ee Mtume wa Allaah].” Akasema: “Niambie au Allaah Mpole na Mwenye khabari zote ataniambia.” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah, namtoa baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako…” Kisha nikamweleza [khabari yote]. Akasema: “Hivi huyo alikuwa wewe, ule mwili mweusi uliokuwa mbele yangu?” Nikasema: “Ndio.” Akanipelekea kidole kifuani mwangu kwa nguvu [akaongeza kwa kusema]: “Je ulidhani kuwa Allaah na Mtume Wake watakukosea?” Nikasema: “Vovote watu watakavyoficha mambo yao basi Allaah atayajua.” [Akasema]: “Ndio. Hakika Jibriyl alinijia uliponiona. Akaniita na akakuficha. Nikaitikia lakini nikakuficha. Haikuwa Jibriyl aingie nyumbani kwako na umevaa nguo zako. Nilidhani umelala na nikachukia kukuamsha na nikaogopa kwamba utajisikia vibaya peke yako. Jibriyl akanambia: ”Hakika Mola wako anakuamuru uwaendee watu wa Baqiy´ na uwaombee msamaha.” Nikasema: ”Niwaambieje, ee Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?” Akasema: ”Sema:
السلام على أهل الديار من المؤمنين والمسلمين، ويرحم الله المستقدمين منا والمستأخرين، وإنا إن شاء الله بكم للاحقون
”Amani iwe juu ya wenyeji wa nyumba hii, miongoni mwa waumini na waislamu, Allaah awarehemu waliotutangulia na watakaokuja nyuma, na sisi – Allaah akitaka – tutakutana nanyi.”
Ameipokea Muslim (3/14) ambaye tamko ni lake, an-Nasaa’iy (1/286; 2/160, 160–161), na Ahmad (6/221). Ziada zote ni zake isipokuwa ya kwanza na ya tatu ambazo ni za an-Nasaa’iy.
Haafidhw ametumia hoja Hadiyth hii katika ”at-Talkhiysw” juu ya kuruhusiwa kwa wanawake kuyatembelea makaburi, nayo ni dalili ya waziwazi. Inaunga mkono kuwa ruhusa hiyo iliwajumuisha wao pamoja na wanaume, kwa sababu kisa hiki kilitokea Madiynah, kwani inajulikana kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimjamii ´Aaishah Madiynah. Katazo hilo mwanzo lilikuwa Makkah. Tuna yakini juu ya hili, ijapokuwa hatujui historia yoyote inayoiunga mkono, kwa sababu makato sahihi yanashuhudia hivo, nayo ni katika maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Nilikuwa nimekukatazeni… ”
Kwa kuwa haifikiriki kwamba katazo hilo lilisuniwa katika zama za Madiynah, badala ya zama za Makkah, ambazo nyingi katika hukumu za Shari´ah zake zilikuwa zinahusiana na Tawhiyd na ´Aqiydah. Katazo la kuyatembelea makaburi ni katika aina hiyo kwa sababu linahusiana na kufunga njia zote inayopelekea katika shirki. Shari´ah yake inafaa zaidi kipindi cha Makkah kwa sababu ndipo watu walipokuwa wakiishi, bado ni wapya katika Uislamu na punde ndio wametoka kuachana na shirki. Ndipo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawakataza kuyatembelea ili isije kuwa njia inayowapelekea katika shirki. Wakati Tawhiyd ilipokita ndani ya nyoyo zao, wakatambua sampuli mbalimbali za shirki zinazopingana nayo, ndipo akawaruhusu kuyatembelea. Hata hivyo kipindi chake chote cha Makkah kuwaacha juu ya desturi yao ya kawaida ya kuzuru na kisha kuwakataza kufanya hivyo huko Madiynah, ni jambo liko mbali sana na hekima ya uwekwaji Shari´ah. Kwa hiyo tuna hakika kwamba katazo hilo liliwekwa huko Makkah. Ikiwa hivyo ndivyo, basi ruhusa yake kwa ´Aaishah kuyatembelea Madiynah ni dalili ya wazi juu ya tuliyoyataja. Zingatia hili, kwa maana ni jambo ambalo limekuwa akilini mwangu, na sijaona mtu yeyote akifafanua kwa namna hii. Ikiwa nimepatia, basi ni kutoka kwa Allaah, na ikiwa nimekosea, basi ni kutoka kwangu mwenyewe[1].
[1] Mtunzi wa kitabu ”Waswiyyat-us-Shar´iyyah”, uk. 26 amejengea hoja hilo kwa kusema:
”Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimkubalia msichana wake Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kutembelea kaburi la ami yake Hamzah (Radhiya Allaahu ´anh).”
ni utumiaji wa dalili batili. Kwa sababu idhini iliyokusudiwa haina msingi wowote katika vitabu vya Sunnah. Naamini si kitu zaidi ya uzushi. Kinachosimuliwa kutoka kwake (Radhiya Allaahu ´anhaa) ni matembezi pekee bila ya kutajwa utolewaji ruhusa kabisa. Ukiongezea ya kwamba hilo halikuthibiti kutoka kwake (Radhiya Allaahu ´anhaa), kwani ni katika mapokezi ya Sulaymaan bin Daawuud, kutoka kwa Ja´far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake ´Aliy bin al-Husayn, kutoka kwa baba yake, kwamba Faatwimah, msichana wake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akizuru kaburi la ami yake Hamzah kila siku ya ijumaa, akiswali na akilia hapo.”
Hivi ndivyo ameipokea al-Haakim (1/377), kupitia njia yake al-Bayhaqiy (4/78) ambaye amesema:
”Hivi ndivyo alivyosema. Imepokelewa pia kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuud, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ja’far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, bila kutajwa ´Aliy bin al-Husayn, kutoka kwa baba yake. Kwa hiyo ni yenye kukatika.”
al-Haakim amesema:
“Wapokezi wake, hadi mwisho wake ni waaminifu.”
adh-Dhahabiy akamraddi kwa kusema: “Hili ni lenye kupingwa sana. Isitoshe Sulaymaan ni dhaifu.”
Mimi nadhani ni Sulayman bin Daawuud bin Qays al-Farra’ al-Madaniy.” Abu Haatim amesema: “Mimi ninamuelewa tu kama inavyopasa.” al-´Azdiy amesema: “Amekosolewa.” Ndio maana adh-Dhahabiy amemjumuisha katika ”adh-Dhwu´afaa” na akaisimulia kauli iliyotajwa hapo juu ya al-´Azdiy. Kwa hivyo msidanganyike na ukimya wa Haafidhw juu ya Hadiyth hii katika ”at-Talkhisw”, uk. 167, ingawa ash-Shawkaniy alimfuata katika hili, kama ilivyo desturi yake katika ”Nayl-ul-Awtwaar”, uk. (4/95). Hata hivyo kwa mujibu wa msimulizi wa kwanza, inasema (´Aliy bin al-Husayn kutoka kwa ´Aliy), hivyo akamwingiza katika cheni ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ilihali ni katika riwaya ya mwanawe al-Husayn (Radhiya Allaahu ´anhumaa), kama ilivyo kwa al-Haakim, au kutoka kwa Ja´far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kama ilivyo katika riwaya ya al-Bayhaqiy ambayo ni pungufu. Pengine yale yaliyomo katika ”at-Talkhisw”, ambayo ni maneno yake “kutoka kwa ´Aliy” ni upotoshaji wa “kutoka kwa baba yake.” Haya yote yameachwa na as-Swan’aniy katika ”Subul-us-Salaam” (2/151), ambaye ameyanasibisha kwa al-Haakim kutoka katika Hadiyth ya ´Aliy bin al-Husayn ya kwamba Faatwimah… Kisha akasema: “Ni Hadiyth ambayo kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi wake, kwa sababu ´Aliy bin al-Husayn hakukutana na Faatwimah bint Muhammad.” Hadiyth hiyo kwa hakika inatokana na Hadiyth ya ´Aliy bin al-Husayn kutoka kwa baba yake, kama ilivyoelezwa hapo awali.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 229-233
- Imechapishwa: 04/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 229-233
Imechapishwa: 04/08/2026
https://firqatunnajia.com/122-dalili-ya-tatu-kufaa-kwa-mwanamke-kuyatembelea-makaburi/