Ibn Abiy Laylaa (afk. 148), Qaadhiy na mwanachuoni wa Kuufah.
143 – Ahmad bin Yuunus amesema:
”Mtu wa kwanza aliyesema kuwa Qur-aan ni kiumbe ni bwana mmoja ambaye Ibn Abiy Laylaa[1] akamtaka atubie, kama alivowataka wakristo kutubia.”[2]
Ibn Abiy Laylaa ni mmoja katika vyombo vya elimu katika Qur-aan, Fiqh na Hadiyth. Hata hivyo wengine wamethibiti zaidi katika Hadiyth kuliko yeye. Baadhi ya wengine wanasimulia kutoka kwake katika yale mapokezi ya mwanzo. Alikuwa ni katika tabaka la Imaam Abu Haniyfah.
Ja´far as-Swaadiq (afk. 148), kiongozi wa watu wa nyumbani kwa ´Aliy katika zama zake na ni mmoja katika maimamu wa Hijaaz. Hata hivyo hakuwahi kukutana na Maswahabah.
144 – Mu´aawiyah bin ´Ammaar amesimulia kuwa Ja´far bin Muhammad aliulizwa kuhusu Qur-aan, ambapo akajibu:
” Sio yenye kuumba wala haikuumbwa; lakini ni maneno ya Allaah (´Azza wa Jall).”[3]
[1] Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Laylaa al-Answaariy al-Kuufiy.
[2] Mtunzi amemsimulia kupitia kwa Ibn Abiy Haatim: al-Husayn bin al-Hasan ametuhadithia: Nimemsikia Ahmad bin Yuunus. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.
[3] Ameisimulia kupitia kwa Abu Zur´ah ar-Raaziy: Suwayd bin Sa´iyd ametuhadithia, kutoka kwa Mu´aawiyah bin ´Ammaar. al-Bayhaqiy ameisimulia kupitia kwa Abu Zur´ah katika “al-Asmaa’ was-Swifaat”, uk. 246. Licha ya kwamba Suwayd bin Sa´iyd al-Hadathaaniy alikuwa ni dhaifu, cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za Muslim. Hata hivyo amefanyiwa ufuatiliaji na Ma´bad bin Raashid Abu ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Mu´aawiyah bin ´Ammaar ad-Duhniy.
- Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 143-144
- Imechapishwa: 21/07/2024
- taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Ibn Abiy Laylaa (afk. 148), Qaadhiy na mwanachuoni wa Kuufah.
143 – Ahmad bin Yuunus amesema:
”Mtu wa kwanza aliyesema kuwa Qur-aan ni kiumbe ni bwana mmoja ambaye Ibn Abiy Laylaa[1] akamtaka atubie, kama alivowataka wakristo kutubia.”[2]
Ibn Abiy Laylaa ni mmoja katika vyombo vya elimu katika Qur-aan, Fiqh na Hadiyth. Hata hivyo wengine wamethibiti zaidi katika Hadiyth kuliko yeye. Baadhi ya wengine wanasimulia kutoka kwake katika yale mapokezi ya mwanzo. Alikuwa ni katika tabaka la Imaam Abu Haniyfah.
Ja´far as-Swaadiq (afk. 148), kiongozi wa watu wa nyumbani kwa ´Aliy katika zama zake na ni mmoja katika maimamu wa Hijaaz. Hata hivyo hakuwahi kukutana na Maswahabah.
144 – Mu´aawiyah bin ´Ammaar amesimulia kuwa Ja´far bin Muhammad aliulizwa kuhusu Qur-aan, ambapo akajibu:
” Sio yenye kuumba wala haikuumbwa; lakini ni maneno ya Allaah (´Azza wa Jall).”[3]
[1] Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Laylaa al-Answaariy al-Kuufiy.
[2] Mtunzi amemsimulia kupitia kwa Ibn Abiy Haatim: al-Husayn bin al-Hasan ametuhadithia: Nimemsikia Ahmad bin Yuunus. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.
[3] Ameisimulia kupitia kwa Abu Zur´ah ar-Raaziy: Suwayd bin Sa´iyd ametuhadithia, kutoka kwa Mu´aawiyah bin ´Ammaar. al-Bayhaqiy ameisimulia kupitia kwa Abu Zur´ah katika “al-Asmaa’ was-Swifaat”, uk. 246. Licha ya kwamba Suwayd bin Sa´iyd al-Hadathaaniy alikuwa ni dhaifu, cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za Muslim. Hata hivyo amefanyiwa ufuatiliaji na Ma´bad bin Raashid Abu ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Mu´aawiyah bin ´Ammaar ad-Duhniy.
Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 143-144
Imechapishwa: 21/07/2024
taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/121-sio-muumba-wala-sio-kiumbe/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)