Dhuriya ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wale wana wake wanaotokamana na Khadiyjah (Radhiya Allaahu ´anhaa), watoto wa Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Wana wa Faatwimah ni wajukuu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yeye ni babu yao. Wana wa Faatwimah na wana wa wana wake na kizazi chao kilichokuja baadaye ni katika watoto wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wana nafasi na cheo maalum kwa sharti wakimfuata na kumwamini. Haitoshi kwa sababu tu ni ndugu zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni lazima kumwamini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wale wanaojenga hoja kwamba ni katika familia yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lakini hawamfuati sio katika kizazi chake hata kama watakuwa ni katika nduguze. Si ndugu zake wote ni katika kizazi chake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mpaka hapa yamemalizika maelezo ya ´Aqiydah ya Imaam na Shaykh Ibn Abiy Zayd (Rahimahu Allaah). Himdi zote njema ni zinamstahikia Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake, Maswahabah zake na wale wenye kuwafuata. Mwisho wa maelezo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 92-93
  • Imechapishwa: 09/09/2021