Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kitu kinachofahamisha hayo ni kitabu cha ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy ambacho alimraddi. ad-Daarimiy alikuwa ni mmoja katika maimamu wanaotambulika aliyekuwa zama za al-Bukhaariy. Ametunga kitabu akakiita ”Radd ´Uthmaan bin Sa´iyd ´alaal-Kaadhib al-´Aniyd”. Humo amenukuu tafsiri hizi mbovu za Bishr al-Mariysiy kwa maneno yanayoonyesha kuwa yeye alikuwa ni mjuzi zaidi kuliko hawa waliokuja nyuma ambao wameyachukua kutoka kwao kutoka upande mwingine. Pale ambapo wenye busara na wenye akili wanaposoma Radd ya ´Uthmaan bin Sa´iyd wataona ni ´Aqiydah ipi waliokuwa nayo Salaf, nguvu ya dalili waliokuwa nayo na unyonge wa dalili ya wale waliokuwa wakipingana nao.
MAELEZO
´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy (Rahimahu Allaah) ni katika maimamu wa Ahl-us-Sunnah na miongoni mwa wanazuoni wa Hadiyth. Alimraddi mchafu huyu Bishr al-Mariysiy kwa Radd kubwa na nzuri na kwa mtindo wenye nguvu. Kitabu hicho kimechapishwa na jina lake ni ”Radd ´Uthmaan bin Sa´iyd ´alaa Bishr al-Mariysiy al-´Aniyd fiymaa iftaraa ´alaa Allaah fiyt-Tawhiyd”. Hii ni katika upole wa Allaah kwamba anawaandalia watu wa batili wale wanaowaraddi na kuwajibu katika kila zama na kila mahali. Hawajali kwa ajili ya Allaah lawama za mwenye kulaumu. Hawawasikilizi wenye kukatisha tamaa na wanaoeneza fitina. Bali wanaendelea mbele katika kubainisha haki na kuraddi batili. Haya ndiyo wajibu wa mwanachuoni, khaswa inapokuwa kuna haja. Hapaswi kunyamaza wala kuwaacha watu wa upotofu waeneze ufisadi ardhini, wawapotoshe watu na waeneze fikira zao. Bali ni wajibu kwa wanazuoni kubainisha na kuwaraddi na kuwajibu hawa watu. Hii ni katika rehema ya Allaah kwamba haukosi wakati wowote kuwepo mwenye kusimama kwa hoja ya Allaah, akiwaraddi watu wa batili na kuinusuru haki na watu wake.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 188-191
- Imechapishwa: 07/07/2026
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kitu kinachofahamisha hayo ni kitabu cha ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy ambacho alimraddi. ad-Daarimiy alikuwa ni mmoja katika maimamu wanaotambulika aliyekuwa zama za al-Bukhaariy. Ametunga kitabu akakiita ”Radd ´Uthmaan bin Sa´iyd ´alaal-Kaadhib al-´Aniyd”. Humo amenukuu tafsiri hizi mbovu za Bishr al-Mariysiy kwa maneno yanayoonyesha kuwa yeye alikuwa ni mjuzi zaidi kuliko hawa waliokuja nyuma ambao wameyachukua kutoka kwao kutoka upande mwingine. Pale ambapo wenye busara na wenye akili wanaposoma Radd ya ´Uthmaan bin Sa´iyd wataona ni ´Aqiydah ipi waliokuwa nayo Salaf, nguvu ya dalili waliokuwa nayo na unyonge wa dalili ya wale waliokuwa wakipingana nao.
MAELEZO
´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy (Rahimahu Allaah) ni katika maimamu wa Ahl-us-Sunnah na miongoni mwa wanazuoni wa Hadiyth. Alimraddi mchafu huyu Bishr al-Mariysiy kwa Radd kubwa na nzuri na kwa mtindo wenye nguvu. Kitabu hicho kimechapishwa na jina lake ni ”Radd ´Uthmaan bin Sa´iyd ´alaa Bishr al-Mariysiy al-´Aniyd fiymaa iftaraa ´alaa Allaah fiyt-Tawhiyd”. Hii ni katika upole wa Allaah kwamba anawaandalia watu wa batili wale wanaowaraddi na kuwajibu katika kila zama na kila mahali. Hawajali kwa ajili ya Allaah lawama za mwenye kulaumu. Hawawasikilizi wenye kukatisha tamaa na wanaoeneza fitina. Bali wanaendelea mbele katika kubainisha haki na kuraddi batili. Haya ndiyo wajibu wa mwanachuoni, khaswa inapokuwa kuna haja. Hapaswi kunyamaza wala kuwaacha watu wa upotofu waeneze ufisadi ardhini, wawapotoshe watu na waeneze fikira zao. Bali ni wajibu kwa wanazuoni kubainisha na kuwaraddi na kuwajibu hawa watu. Hii ni katika rehema ya Allaah kwamba haukosi wakati wowote kuwepo mwenye kusimama kwa hoja ya Allaah, akiwaraddi watu wa batili na kuinusuru haki na watu wake.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 188-191
Imechapishwa: 07/07/2026
https://firqatunnajia.com/120-ruduud-rehema-kutoka-kwa-allaah/