120. Kitenguzi cha nane: Kuwasaidia washirikina dhidi ya waislamu

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

La nane:

Kuwasaidia washirikina dhidi ya waislamu. Dalili ni maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

”Yeyote atakayewafanya vipenzi, basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.” (al-Maaidah 05 :51)

MAELEZO:

Shaykh (Rahimahu Allaah) amechukua aina moja katika aina za kujenga urafiki na makafiri. Nako ni kule kuwasaidia. Vinginevyo ni kwamba ´kuwafanya marafiki` kunajumuisha kuwapenda moyoni, kuwasaidia dhidi ya waislamu, kuwasifu makafiri na mengineyo. Kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewawajibishia waislamu kuwachukulia makafiri kama maadui, kuwachukia na kujitenga mbali nao. Haya ndio yale ambayo katika Uislamu yanaitwa ´kuwapenda waislamu na kuwachukia makafiri`.

Kuwasaidia makafiri… – Kuwasaidia ndio maana ya Mudhwaaharah. Kisha akastadili (Rahimahu Allaah) kwa Aayah:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ

”Enyi mlioamini! Msiwachukuwe mayahudi na manaswara kuwa ndio marafiki vipenzi – wao kwa wao ni marafiki vipenzi. Yeyote atakayewafanya marafiki, basi hakika yeye ni miongoni mwao.” (al-Maaidah 05:51)

Hapa kuna dalili ya ukafiri kwa yule mwenye kufanya hivyo. Kwa sababu udhahiri wa maneno Yake:

فَإِنَّهُ مِنْهُمْ

“… basi hakika yeye ni miongoni mwao.”

bi maana yeye ni mfano wao katika ukafiri. Hii ndio sababu ya Shaykh (Rahimahu Allaah) kutumia Aayah hii kama dalili.

Kama tulivyosema ya kwamba ´kujenga urafiki` kumegawanyika aina mbalimbali. Miongoni mwa kuwafanya marafiki ni pamoja na  kuwapenda moyoni japokuwa mtu hatodhihirisha hayo, kuwasaidia, kuwanusuru, kuwasifu na kuitapa dini yao. Yote haya yanaingia katika neno ´kuwafanya marafiki`.

وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ

“Yeyote atakayewafanya marafiki, basi hakika yeye ni miongoni mwao.”

Akawafanya marafiki kwa kuwapenda, kuwanusuru, kuwasaidia na kuwasifu. Aayah hii ni yenye kuenea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 158-159
  • Imechapishwa: 18/02/2019