Haafidhw Hammaad bin Zayd al-Baswriy (98-179), mmoja katika wanazuoni wakubwa.

141 – Sulaymaan bin Harb amesimulia kuwa amemsikia Hammaad bin Zayd akisema:

”Hakika si vyengine ni kwamba wanazungukia kusema kuwa hakuna Mungu juu ya mbingu.”[1]

Bi maana Jahmiyyah.

´Aqiydah ya Salaf na ya Ahl-us-Sunnah, na bali mpaka ya Maswahabah, ya Allaah, ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ya waumini, wanasema kwamba Allaah (´Azza wa Jall) yuko juu ya mbingu na juu ya ´Arshi, kwamba ´Arshi Yake iko juu ya mbingu Zake na kwamba hushuka katika mbingu ya chini kabisa. Dalili yao juu ya hayo ni Maandiko na masimulizi.

Upande wa pili ni kwamba Jahmiyyah wanasema kuwa Allaah yuko kila mahali. Allaah ametakasika kutokana na ´Aqiydah yao! Bali Yeye yupamoja nasi kwa utambuzi Wake.

Wale wanafalsafa waliokuja nyuma wanasema kuwa Allaah hana mahali na kwamba Allaah (Ta´ala) hayuko si juu ya mbingu, juu ya ´Arshi, juu ya ardhi, ndani ya ulimwengu, nje ya ulimwengu, hakutengana na viumbe Wake na wala hakushikana nao. Aidha wanasema kuwa vyote vilivyotajwa ni sifa za viwiliwili – na kwamba Allaah (Ta´ala) ametakasika kutokana na kiwiliwili. Ndipo Ahl-us-Sunnah wakawajibu kwa kuwaambia kuwa hatupekui katika mambo hayo. Tunasema tu yale yaliyotajwa ndani ya Maandiko. Ikiwa nyinyi mnadai… Sisi hatusemi kile mnachokisema. Kile mnachokisema ni sifa za kitu kisichokuwepo. Allaah ametakasika kutokana na kutokuwepo. Bali Yeye yuko na Ametengana na viumbe Wake na Anasifika kwa yale aliyojisifu Mwenyewe, kukiwemo kwamba Yuko juu ya ´Arshi. Hata hivyo haitakiwi kumfanyia namna.

Inapokuja katika utukufu na elimu, Hammaad bin Zayd watu wa ´Iraaq ni kama Maalik bin Anas kwa watu wa Hijaaz.

142 – Abun-Nu´maan ´Aarim amesimulia kutoka kwamba Hammaad bin Zayd aliyesema:

”Qur-aan ni maneno ya Allaah. Jibriyl ameshuka nayo kutoka kwa Mola wa walimwengu.”

Ameipokea mtoto wa Ahmad katika ”as-Sunnah”[2].

[1] Mtunzi ametaja ile iliyosimuliwa na Haafidhw Abu Haatim ar-Raaziy katika “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”. ´Abdullaah bin Ahmad pia ameipokea katika ”as-Sunnah”, uk. 09-10, kupitia njia mbili kutoka kwa Sulaymaan bin Harb. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh na imesahihishwa na Ibn Taymiyyah katika ”al-Hamawiyyah”.

[2] Huko amesema kuwa ”nimekhabarishwa kutoka kwa Abun-Nu´maan”, uk. 25.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 143
  • Imechapishwa: 21/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy