Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

7- Haangamii wala hatoweki.

MAELEZO

Kuangamia na kutoweka kuna maana moja. Allaah (Subhaanah) ni Mwenye kusifiwa kwa uhai wenye kubaki na wenye kudumu. Amesema (Ta´ala):

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ

”Mtegemee Aliye hai ambaye hafi.”[1]

Haangamii. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

وكُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kuangamia isipokuwa uso Wake.”[2]

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

”Utabakia uso wa Mola wako wenye utukufu na ukarimu.”[3]

Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ni Mwenye kubaki ilihali viumbe watakufa na kisha baadaaye watafufuliwa. Hapo mwanzoni hawakuwepo ambapo Allaah akawaumba. Kisha watakufa na hatimaye Allaah (Jalla wa ´Alaa) atawafufua. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hana mwanzo wala mwisho.

[1] 25:58

[2] 28:88

[3] 55:27

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 13/06/2019