12. Sura ya tatu: Ubainifu wa unyenyekeaji wa ulimwengu katika ujisalimishaji na kumtii Allaah

Ulimwengu wote – kukiwemo mbingu, ardhi, sayari, nyota zake, viumbe, miti, mawe, nchikavu, bahari, Malaika, majini na watu wake – vyote ni wenye kumnyenyekea Allaah na ni vyenye kutii amri Yake ya kilimwengu. Amesema (Ta´ala):

وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا

“… na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende.”[1]

بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ

“Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini – vyote vinamtii.”[2]

وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ

“Ni kwa Allaah pekee vinasujudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini katika viumbe vitembeavyo, na Malaika, nao hawatakabari.”[3]

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَسْجُدُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ النَّاسِ

”Je, huoni kuwa wanamsujudia Allaah walioko mbinguni na ardhini, na jua, na mwezi na nyota, na milima na miti na viumbe vinavyotembea, na wengi miongoni mwa watu?”[4]

وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَظِلَالُهُم بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ

“Kwa Allaah pekee vinamsujudia vilivyomo mbinguni na ardhini – wakipenda wasipende – na vivuli vyao pia [vinamsujudia] asubuhi na jioni.”[5]

Viumbe vyote hivi ni vyenye kujisalimisha na kunyenyekea ufalme Wake. Zinatembea kutokana na matakwa Yake na kutii amri Yake. Hakuna chochote katika hivyo kinachoasi. Vinasimama kwa kazi zake, kutekeleza natija zake kwa mpangilio mzuri na ametakasika muumbaji wavyo kutokamana mapungufu, kushindwa na kasoro. Amesema (Ta´ala):

تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ

“Zinamsabihi mbingu saba na ardhi na vilivyomo ndani yake na hakuna kitu chochote isipokuwa kinamtukuza kwa himdi Zake, lakini hamzifahamu Tasbiyh zao.”[6]

Viumbe hivi – kukiwemo vile vilivyo kimya na vinavyotamka, vilivyohai na vilivyokufa – vyote ni vyenye kumtii Allaah na ni vyenye kunyenyekea amri Yake ya kilimwengu. Vyote ni vyenye kumtakasa Allaah kutokamana na mapungufu na kasoro kutokana na mazingira yao na misemo yao. Kila ambavyo mwenye akili atazingatia juu ya viumbe hivi atatambua kuwa vimeumbwa kwa haki na kwa ajili ya haki na kwamba ni wenye kuendeshwa na havijiendeshi na havitoki nje ya amri ya mwendeshaji Wake. Kwa hiyo vyote kwa maumbile yao ni vyenye kumkiri muumbaji. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ni vyenye kunyenyekea na vyenye kujisalimisha, vyenye kutii na vyenye kutenzwa nguvu, kwa njia mbalimbali:

  • Kutambua kwao haja zao na udharurah wao Kwake.
  • Kunyenyekea na kujisalimisha kwavyo kutokana na makadirio na matakwa Yake yanayowapitikia.
  • Vinamuomba Yeye wakati wanapolazimika.

Muumini ananyenyekea amri ya Allaah kwa kupenda kwake na kadhalika kutokana na ile misiba anayomkadiria. Inapomfika basi anafanya yale aliyomwamrisha katika kusubiri na mengineyo hali ya kupenda kwake mwenyewe. Kwa hivyo anakuwa ni mwenye kujisalimisha kwa Allaah na mwenye kunyenyekea Kwake kwa kupenda kwake mwenyewe.”[7]

Kafiri pia ananyenyekea juu ya amri ya Allaah ya kilimwengu. Viumbe kusujudu kinachokusudiwa ni kule kunyenyekea kwavyo. Kila kitu kinasujudu kutokana na hali yake na ni sujudu inayonasibiana na kitu hicho ambayo ndani yake mna kumnyenyekea Mola. Kila kitu kinamtukuza kulingana na hali yake na ni jambo la ukweli na si la mafumbo.”

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ

“Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi – akipenda asipende – na Kwake watarudishwa.”[8]

“Ametaja (Subhaanah) ujisalimisha wa viumbe kwa kupenda na kutokupenda. Kwa sababu viumbe vyote ni vyenye kumwabudu ´ibaadah timilifu. Ni mamoja mwenye kukubali atayakubali hayo au asiyakubali. Wao ni wenye kuendeshwa Naye. Wao ni wenye kujisalimisha Kwake kwa kupenda na kutokupenda. Hakuna yeyote katika viumbe wake anayetoka nje ya yale aliyotaka, akayakadiria na kuyapanga. Hakuna hila wala namna isipokuwa kwa msaada Wake. Yeye ndiye Mola wa walimwengu na mfalme  Wao anayewaendesha vile anavyotaka. Yeye ndiye kawaumba wote, mungu na muumbaji wao. Kila asiyekuwa Yeye ni mwenye kuendeshwa, aliyeumbwa, fakiri, muhitaji, mja na dhalili. Upande mwingine Yeye (Subhaanah) ni mmoja, mwenye kudhibiti na kudhalilisha, muumbaji na mwendeshaji, mwanzilishi viumbe na muundaji sura na umbile.”[9]

[1] 03:83

[2] 02:116

[3] 16:49

[4] 22:18

[5] 13:15

[6] 17:44

[7] Majmuu´-ul-Fataawaa (01/45).

[8] 03:83

[9] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/200).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 30-32
  • Imechapishwa: 05/02/2020