08 – Mume kufanya haraka kutoa talaka
Baadhi ya waume hawana subira na utulivu wa mambo. Wanakuwa ni wepesi wa hasira na ghadhabu. Kwa hakika mwanaume kama huyu anahitaji kufunga mdomo wake na ajifunze upole, utulivu na subira. Aidha anapaswa kutambua kuwa maisha yote haya ya ndoa hayakutandikwa waridi na maua, kijani kibichi na ardhi laini. Hakika mambo yalivyo ni kwamba kuna miiba, vijibonde na milima njiani. Kwa hivyo mwanaume awe ile nafasi ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amemuweka. Asifanye haraka na asikasirike. Badala yake awe mtu mwenye upole na mwenye subira, kufanya mambo kwa utulivu na mwenye kumuomba Allaah msaada. Asifanye haraka, kwani haraka haileti kheri yoyote. Ee mja wa Allaah, muda wa kuwa Allaah ameiweka talaka mikononi mwako basi kuwa kwa kadri ya kile kiwango cha kubeba jukumu.
- Muhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 27-28
- Imechapishwa: 05/04/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)