12. Qur-aan kwa mujibu wa Ashaa´irah

Ashaa´irah wanasema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah yaliyosimama kwenye dhati Yake na hayana herufi wala sauti. Kwa mujibu wao Qur-aan tulio nayo sio maneno ya Allaah. Wanachotaka kusema kuwa maneno ya Allaah ni maana ya ndani iliyosimama kwenye dhati ya Allaah. Kwa mujibu wao ndio Qur-aan, Tawraat na Injiyl. Akiizungumza kwa kwa kiebrania, inakuwa ni Tawraat. Akiizungumza kwa kisyria, inakuwa ni Injiyl. Akiizungumza kwa kiarabu, inakuwa ni Qur-aan.

Wanaonelea kuwa Qur-aan kwa maamrisho, makatazo na maelezo yake ni maana moja isiyogawanyika. Nadharia yao ni ya kipumbavu na batili na hayakubaliwi si na akili wala Shari´ah. Allaah kuzungumza kunafahamisha ukamilifu. Kuna tofauti kubwa kati ya mwenye kuzungumza na bubu. Bubu ni mpungufu. Yule ambaye Allaah amemtunuku kuzungumza ni mkamilifu zaidi kuliko bubu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 15/10/2016