12. Mfano wa tatu wa hekima ya Mtume (صلى الله عليه وسلم)

Kuhusu mtu aliyechemua ndani ya swalah. Kisa hicho kimesimuliwa na Mu´aawiyah bin al-Hakam (Radhiya Allaahu ´anh) ambapo kuna mtu alijiunga na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah ambapo akapiga chafya na kusema:

الحمد لله

“Hidmi zote anastahiki Allaah.”

Mu´aawiyah akamwambia:

يرحمك الله

“Allaah akurehemu.”

Watu wakamkazia macho wakiwa ni wenye kumkemea kwa maneno yake. Akasema: “Mna nini mbona mnanitazama namna hiyo?” Wakaanza kupiga mapaja yao. Nilipoona hivo nikanyamaza. Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomaliza kuswali akanielekea na kunikaribia na sijawahi kuona hapo kabla wala baada mafunzo yaliyo mazuri kabisa kuliko yake. Ninaapa kwa Allaah! Hakunilazimisha, hakunipiga wala hakunambia vibaya. Alisema: “Hakika swalah hii hakufai kitu katika maneno ya watu. Ndani yake mna Tasbiyh, Takbiyr na kusoma Qur-aan.”

Au Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema maneno mfano wa hayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017