Abu Mu´aadh al-Balkhiy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Allaah yuko juu ya mbingu juu ya ´Arshi, kama alivyojisifia Mwenyewe.”[1]

Hudbah bin Khaalid ametuhadithia: Nimemsikia Salaam bin Abiy Mutwiy´ akisema:

”Ole wenu kwa kupinga kwenu jambo hili! Naapa kwa Allaah! Hakuna chochote katika Hadiyth isipokuwa ndani ya Qur-aan kuna kinachothibitisha zaidi. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ

”Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[2]

وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ

“Na Allaah anakutahadharisheni nafsi Yake.”[3]

تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ

”Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu na wala mimi sijui yale yaliyomo katika nafsi Yako.”[4]

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ الْعَالَمِينَ

”… kisha akalingana juu ya ´Arshi.”[5]

وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ

”Na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume.”[6]

مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Kipi kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?”[7]

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

”Na bila shaka Allaah alimzungumzisha Muusa maneno kihakika.”[8]

يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي

”Ee Muusa! Hakika Mimi nimekuteua juu ya watu kwa Ujumbe na maneno Yangu.”[9]

Aliendelea kuzungumzia hilo kuanzia wakati wa ´Aswr mpaka kuzama kwa jua.”[10]

Ameipokea Ibn Abiy Haatim kupitia kwa Abu Zur´ah, kutoka kwa Hudbah.

Yaziyd bin Haaruun amesema:

“Wale wenye kusema kuwa Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi kwa namna isiyofahamika na kile kilicho imara katika mioyo ya watu wa kawaida, huyo ni Jahmiy.”[11]

Ameipokea ´Abdullaah bin Imaam Ahmad katika ”as-Sunnah”.

Hayo yamesemwa pia na ´Abdullaah bin Maslamah al-Qa´nabiy, mwalimu wa al-Bukhaariy na Muslim. Bayaan bin Ahmad amesema:

”Tulikuwa kwa ya al-Qa´nabiy wakati alipomsikia mtu mmoja katika Jahmiyyah akisema kwamba mwingi wa Rehema ametawala (استولى) juu ya ´Arshi. Ndipo al-Qa´nabiy akasema: “Yeyote asiye na yakini kwamba mwingi wa Rehema amelingana juu juu ya ´Arshiy amestawi kama inavyokubalika katika nyoyo za watu wa kawaida, basi huyo ni Jahmiy.”[12]

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Mukhtaswar-ul-´Uluww” (171).

[2] 31:28

[3] 03:30

[4] 05:116

[5] 07:54

[6] 39:67

[7] 38:75

[8] 04:164

[9] 07:144

[10] Cheni ya wapokezi Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Mukhtaswar-ul-´Uluww” (90).

[11]Ameipokea ´Abdullaah bin Ahmad katika “as-Sunnah”, uk. 11-12, na kupitia kwake ameisimulia mtunzi wa kitabu. Hapa, na maeneo mengine, ametaja kitabu chake “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” na akasema: ´Abdullaah amesema: ´Abbaas bin ´Abdil-´Adhwiym al-´Anbariy amenihadithia: Shaadh bin Yahyaa  ametuhadithia…

Abu Daawuud ameipokea katika “Masaa’il-ul-Imaam Ahmad”, uk. 268, na akasema: Ahmad bin Sinaan ametuhadithia: Nimemsikia Shaadh bin Yahyaa…

Cheni hii ya wapokezi ni nzuri. Kuna watu wengi madhubuti wamenukuu kutoka kwa Shaadh bin Yahyaa na Ahmad pia alimzungumzia kwa wema. al-Bukhaariy ameyanukuu masimulizi haya kwa cheni ya wapokezi pungufu na akasema:

”Yaziyd bin Haaruun alitawahadharisha Jahmiyyah na akasema: “Wale wenye kusema kuwa mwingi wa Rehema amelingana juu ya ´Arshi kwa namna isiyofahamika na kile kilicho imara katika mioyo ya watu wa kawaida, huyo ni Jahmiy.” (Khalqu Af´aal-il-´Ibaad (63))

[12] Cheni ya wapokezi ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Mukhtaswar-ul-´Uluww” (182).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 55-57
  • Imechapishwa: 23/12/2025