12. Du´aa ya kujilinda kwa Allaah na uvivu, madhambi, madeni, mtihani wa kaburi n.k.

51 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْكَسَلِ وَالْهَرَم، وَالْمَالَم وَالْمَغْرَم وَمِنْ فِتْنَةِ الْقَبْر وَعَذَابِ الْقَبْر، ومن فتنة النَّارِ وَعَذَابِ النَّارِ، وَمِنْ وَمِنْ فِتْنَةِ شَرِّ فِتْنَةِ الْغِنَى وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْفَقْرِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ ، فِتْنَةِ الْمَسِيحَ الدَّجَّالِ اللَّهُمَّ السِلَ عَنِّي خَطَايَايَ بِمَاءِ التَّلْجِ وَالْبَرَدِ، وَنَةٌ قَلبي مِنْ الْخَطَايَا كَمَا نَقَيتَ الثوب الأبيض مِن الدَّنَسِ، وَبَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ

“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokana na uvivu, uzee, madhambi, madeni, kutokana na mtihani na adhabu ya kaburi, kutokana na mtihani na adhabu ya Moto, shari ya mtihani wa utajiri na najilinda Kwako kutokana na mtihani wa al-Masiyh ad-Dajjaal. Ee Allaah! Nioshe makosa yangu kwa maji ya theluji na barafu na utakase moyo wangu na makosa kama kama Ulivyoitakasa nguo nyeupe kutokamana na uchafu, nitenge mbali mimi na makosa yangu kama Ulivyotenga mbali kati ya mashariki na magharibi.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Du´aa hii imekusanya du´aa hizi tukufu ambazo muislamu anatakiwa kuziomba ndani na nje ya swalah.

Uvivu ni kuchelewesha kitendo licha ya kwamba mtu ana uwezo wa kukifanya akiegemea starehe.

Uzee kunakusudiwa umri wenye udhalili.

Madhambi (الْمَأْثَم) ni yale yanayopelekea katika madhambi.

Madeni yanamfanya mtu kusumbuliwa na kutafutwa.

Mtihani wa kaburi ni maswali ya Malaika wawili pale wanapomuhoji kuhusu Mola, dini na Mtume Wake.

Mtihani wa Moto imesemekana kuwa ni maswali ya mlinzi wa Moto kwa njia ya makemeo. Maoni mengine yanasema kuwa ni yale matendo yanayomsababishia mtu kuingia Motoni.

Shari ya mtihani wa utajiri ni yale yanayotokana na jambo hilo kukiwemo maovu, kiburi, dhuluma, kuichuma kwa njia ya haramu na kuitoa kwa yale ambayo hayakuwekwa katika Shari´ah na Allaah.

Mtihani wa ufukara ni yale yanayotokana na jambo hilo kukiwemo kukata tamaa, kukasirika na kutokuwa na subira. Aidha ufukara wakati mwingine unampelekea mtu kufanya mambo ya haramu kama vile mtu kuahidi kisha akavunja ahadi yake.

Kukoshwa makosa kunakusudiwa yasamehewe.

Kutakaswa kwa maji yenye theluthi na baridi kunakusudiwa yanafanyika hayo baada ya maji, jambo ambalo linasafisha zaidi.

Moyo kutakaswa kutokana na makosa kunakusudiwa moyo kusamehewa, kusitiriwa na kulindwa.

Kutengwa mbali na makosa kama umbali kati ya mashariki na magharibi kunakusudiwa kusalimishwa kutokana madhambi kwa mtu kuwekwa mbali. Mtu akitengwa mbali masafa haya basi anasalimika nayo.

[1] al-Bukhaariy (6358) na Muslim (589).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 58
  • Imechapishwa: 15/10/2025