12. al-Halabiy anamtuhumu Rabiy´ al-Madkhaliy kuwatukana wanachuoni

al-Halabiy amesema:

“Kujigonga kwa Shaykh Rabiy´al-Madkhaliy hakukukomeka tu na elimu na tabia yake. Inahusiana vilevile na kujigonga maneno yake. Mfano wa hilo ni yale niliyoandika kwenye makala yangu inayoitwa “Twu´uwnaat-ush-Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy wa Kibaar A´waanihi bis-Salafiyyiyn – ´Ulamaa-an wa Du´aatan”. Humo nimeandika:

Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy anapinga kuwa amewatukana baadhi ya watu ambao amewatukana kikweli katika vikao vyake binafsi (kama ambavyo mtakuja kusikia kwenye kipande hichi). Ilikuwa wakati anajibu swali katika mnasaba wa “al-Mukhayyam ar-Rabi´i”. Humo anasema muulizaji:

“Anasema kuwa Shaykh Rabiy´ anawatukana wanachuoni sawa wa zamani na wa sasa. Anasema kuwa Dr Rabiy´ bin Haadiy amesema ya kwamba Ibn Baaz ameiponda Salafiyyah vibaya sana, ambalo amelinukuu kutoka “al-Faswl al-´Aadil”. Anasema pia kuwa amemtukana Ibn Hajar na an-Nawawiy, amemfanyia Tabdiy´ Shu´bah, amemtuhumu Imaam Ahmad bin Hanbal kuwa alipotosha baadhi ya Sifa za Allaah, amesema kuwa Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab alikuwa ni kijana mpotevu, amemtuhumu Ibn Khuzaymah kuwa amepotosha baadhi ya Sifa za Allaah, amesema kuwa Ibn ´Uthaymiyn ndiye sababu ya shirki inayopatikana Najd, amesema kuwa Salafiyyah yao ni yenye nguvu zaidi kuliko Salafiyyah ya al-Albaaniy, kwamba Shu´bah ni mtu wa Bid´ah, Sufyaan ath-Thawriy alijitupa kati ya Raafidhwah na kwamba Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab alikuwa na hamasa na misukumo ya kijana. Yote haya yananasibishwa kwako na yametolewa “al-Faswl al-´Aadil”.

Jibu: Ametakasika Allaah. Huu ni uongo mkubwa. Hivi hapa vitabu na kanda zangu. Havina isipokuwa ni utetezi kwa maimamu wa Ahl-us-Sunnah kukiwemo hao uliyowataja.”[1]

1 – Sina kujigonga inapokuja katika elimu wala tabia. Hii ni sifa yako wewe na pote lako.

2 – Sikuwatukana Salafiyyuun, nimeraddi tu upotevu wa watu wa Bid´ah. Wao hawana wanachuoni. Walicho nacho ni watu tu wanaoita katika fitina na kusababisha ghasia kati ya Ahl-us-Sunnah.

3 – Mnasema uongo. Sijawatukana wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah si wa zamani wala wa sasa. Ninaita watu kwao na kuwaamrisha watu kuwaheshimu na kuwafuata.

4 – al-Halabiy hatosheki na uongo wake kwangu; anaenda pia kuleta uongo wa Haddaadiyyah na upotoshaji wao na kufasiri maneno yangu kwa tafsiri zisizokubaliwa.

Msimamo wangu kwa wanachuoni wa zamani na wa sasa na kuwatetea na kuita katika mfumo wao kunaponda uongo na uzushi wa al-Halabiy na Haddaadiyyah.

[1] Uk. 01

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
  • Imechapishwa: 08/01/2017