11. Rabiy´ al-Madkhaliy hakupendekeza kitabu “al-Ibaanah” cha Muhammad al-Imaam

al-Halabiy amesema:

“Badala ya Shaykh Rabiy´ kukabiliana na kitabu hiki kama jinsi alivokabiliana na “Manhaj-us-Salaf as-Swaalih” kwa radd, marudisho, vurugu na chokochoko, akakabiliana nacho kinyume kabisa! Kitabu alikisoma na akaweka baadhi ya taaliki na ambapo Shaykh al-Imaam akaandika kwenye ukarasa wa kwanza:

“Kimesomwa na muheshimiwa Shaykh na ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy”

Sababu ya hilo ni kwamba Shaykh Rabiy´ aliona kuwa malengo ya kitabu “al-Ibaanah” ilikuwa ni Radd kwa Shaykh al-Hajuuriy ambaye Shaykh Rabiy´ alimvumilia na kumnasihi. Shaykh al-Madkhaliy anakubaliana na kauli na kinyume chake yote mawili, kusifu kauli na kuikataa. Haangalii kinachosemwa, anachoangalia ni nani mwenye kusema. Hili limefanya Shaykh al-Madkhaliy kutumbukia katika kujigonga na kitendawili.”[1]

Mimi sikupendekeza kabisa kitabu cha al-Imaam “al-Ibaanah”. Kwanza nilisoma tu baadhi ya kurasa na nikakemea baadhi ya mambo. Niliweka taaliki kwa lengo la kumzindua Muhammad al-Imaam ili aweze kujirudi makosa yake. Halafu nikakisoma kwa mara ya pili na nikaashiria baadhi ya makosa katika kitabu hichi. Nikamtaka al-Imaam ajirudi katika makosa haya na akikague tena kitabu chake. Akiona makosa yanayoenda kinyume na mfumo wa Salaf ni lazima ajirudi. Bado ningali katika msimamo huu huu na kuupa kipaumbele:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّـهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ

“Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu mtoapo ushahidi kwa ajili ya Allaah japokuwa ni dhidi ya nafsi zenu au wazazi wawili, au jamaa wa karibu.” (04:135)

Kujigonga kuko wapi na khaswa ukizingatia ya kwamba wewe mwenyewe umekiri kuwa niliweka taaliki?

Mimi naraddi batili kwa kuwa ni batili. Tofauti na unavyonizushia sikubaliani na batili. Ushahidi wa wanachuoni, na khaswa al-Albaaniy, juu ya kwamba vitabu vyangu ni sahihi na vinaraddi batili na haviendi kinyume na mfumo wa Salaf unatosheleza kufichua ujinga na dhuluma zako. Dhuluma zako, ujinga wako na chuki zako zinakufanya kuona haki kuwa ni batili na batili kuwa ni haki.

[1] Uk. 01

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
  • Imechapishwa: 08/01/2017