119. Kitabu kibaya zaidi katika mada hii

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Upindishaji mwingi wa maana uliopo hii leo kama vile wa Abu Bakr bin Furaak na Abu ´Abdillaah Muhammad bin ´Umar ar-Raaziy ambao ameutaja katika kitabu chake “Kitaab-ut-Ta´wiylaat” na “Ta´siys-ut-Taqdiys”. Nyingi katika tafsiri mbovu hizi zinapatikana kwa watu kama vile Abu ´Aliy al-Jubbaa´iy, ´Abdul-Jabbaar bin Ahmad al-Hamadaaniy, Abul-Husayn al-Baswriy, Abu Wafaa’ bin ´Aqiyl na Abu Haamid al-Ghazaaliy.Tafsiri mbovu kama hizo ndizo zinazotumiwa na Bishr al-Mariysiy katika kitabu chake. Ingawa katika maneno ya baadhi ya hawa waliyotajwa kunaweza kupatikana wakiraddi na kubatilisha tafsiri mbovu na wakiandika maneno mazuri juu ya baadhi ya mada. Ninacholenga ni kwamba ukweli wa mambo tafsiri zao ni zilezile za al-Mariysiy.

MAELEZO

Upindishaji wa maana (التأويلات) wakati fulani hutumika kumaanisha tafsiri, wakati mwingine hutumika kama kuligeuza tamko kutoka katika dhahiri yake, na hili ndilo limekusudiwa hapa, na mara nyingine pia hutumika kwa maana ya yale ambayo jambo litarejea kwake mwishoni. Shaykh anakusudia maana ya pili, nayo ni kuligeuza tamko kutoka katika dhahiri yake, kwa sababu wao waliyageuza maandiko kutoka katika dhahiri yake na wakasema kuwa dhahiri yake haikusudiwi. Bali zinakusudiwa maana nyingine au kwamba hakuna anayejua maana yake isipokuwa Allaah tu. Haya ndio madhehebu ya watu wa upotovu.

Fakhr-ud-Diyn ar-Raaziy alikuwa mfasiri wa Qur-aan. Anacho kitabu kwa jina “Ta´siys-ut-Taqdiys” ambacho ndani yake amekusanya tafsiri mbovu ambazo anaziitakidi na kuziamini. Hivyo ni kitabu kibaya zaidi katika mada hii. Shayk-hul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) akakiraddi kwa kitabu kikubwa kwa jina ”Naqdhw-ut-Ta’siys”. Hicho ni miongoni mwa tungo bora kabisa za Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

Shaykh anachotaka kusema ni kuwa katika maneno ya hawa watu kuna sehemu ya kheri na haki. Haifai ikiwa mtu ana mema na ana kheri tukafumbia macho batili na upotofu uliopo kwake. Bali ni lazima kubainisha hayo. Wala tusiathiriwe na na wale wanaosema ”haki sawa” (الموازنة). Wanachotaka ni sisi kufumbia macho makosa yaliyopo kwa baadhi ya watu. Huu ni udanganyifu kwa waislamu na ni kuieneza batili.

Tafsiri mbovu zilizopo katika vitabu vya Ashaa´irah, Mu´tazilah na vya Maturidiyyah ndio tafsiri mbovu zilezile za al-Mariysiy, ambaye ndiye kiongozi wa upotofu.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 188-191
  • Imechapishwa: 07/07/2026

Turn on/off menu