119. Du´aa siku ya ´Arafah

  Download

237- Du´aa bora ni du´aa ya siku ya ´Arafah. Bora nilichosema mimi na Mitume wengine kabla yangu ni:

لا إِلَهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَريكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ ولَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدير

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake, himdi zote njema ni stahiki Yake, Naye juu ya kila jambo ni muweza.”[1]

[1] at-Tirmidhiy (3585). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/184) na katika ”al-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (04/6).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 08/05/2020