138 – Abu Zur´ah ar-Raaziy amesema: Hudbah bin Khaalid ametuhadithia: Nimemsikia Salaam bin Abiy Mutwiy´ akisema:

”Ole wenu kwa kupinga kwenu jambo hili! Naapa kwa Allaah! Hakuna chochote katika Hadiyth isipokuwa ndani ya Qur-aan kuna kinachothibitisha zaidi. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ

”Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[1]

وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ

“Na Allaah Anakutahadharisheni nafsi Yake.”[2]

تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ

”Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu na wala mimi sijui yale yaliyomo katika nafsi Yako.”[3]

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ الْعَالَمِينَ

”… kisha akalingana juu ya ´Arshi.”[4]

وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ

”Na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume.”[5]

مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Kipi kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?”[6]

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

”Na bila shaka Allaah alimzungumzisha Muusa maneno kihakika.”[7]

يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي

”Ee Muusa! Hakika Mimi nimekuteua juu ya watu kwa Ujumbe na maneno Yangu.”[8]

Aliendelea kuzungumzia hilo kuanzia wakati wa ´Aswr mpaka kuzama kwa jua.”[9]

Hammaad bin Salamah (afk. 167), imamu wa watu wa Baswrah.

90 – Alikuwa (Rahimahu Allaah) ni katika maimamu wa Ahl-us-Sunnah, mmoja katika wale walioeneza Hadiyth zinazozungumzia sifa, kiongozi katika elimu na matendo. ´Abdul-´Aziyz bin al-Mughiyrah[10] amesema:

”Hammaad bin Salamah ametuhadithia Hadiyth kuhusu kushuka kwa Mola (´Azza wa Jall), kisha akasema: ”Mtakayemuona anaikanusha basi mtuhumuni.”

[1] 31:28

[2] 03:30

[3] 05:116

[4] 07:54

[5] 39:67

[6] 38:75

[7] 04:164

[8] 07:144

[9] Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Mtunzi amesimulia kupitia kwa Abu Zur´ah ar-Raaziy, kutoka kwa Hudbah bin Khaalid: Nimemsikia Salaam bin Abiy Mutwiy´.

[10] Abu ´Abdir-Rahmaan ´Abdul-´Aziyz bin al-Mughiyrah as-Swaffaar al-Munqariy alikuwa ni mkweli.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 140-141
  • Imechapishwa: 17/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy