al-Layth bin Sa´d (afk. <175), mwanachuoni wa Misri.
137 – Mtunzi amesimulia kutoka kwa al-Waliyd bin Muslim, ambaye amesema:
”Nilimuuliza al-Awzaa´iy, al-Layth bin Sa´d, Maalik na ath-Thawriy juu ya Hadiyth zinazozungumzia Kuonekana na nyenginezo. Wakasema: ”Zipitisheni bila ya kuzifanyia namna.”[1]
[1] Imeshatangulia punde kidogo kwa tamko lisemalo:
”Zipitisheni kama zilivyokuja bila ya tafsiri.”
Ibn Taymiyyah amesema:
”Kusema kwamba Hadiyth zipitishwe kama zilivyokuja kuna Radd dhidi ya Wakanushaji. Kusema kwamba zipitishwe bila ya kuzifanyia namna kuna Radd dhidi ya Wafananishaji.” (al-Hamawiyyah)
Ibn-ul-Qayyim amesema:
”Makusudio ya Salaf ”bila ya kuzifanyia namna” ni kukanusha kupindisha maana. Wapindishaji wanadai kupindisha maana, kwa sababu wao ndio wenye kuthibitisha namna inayopingana na uhakika na hivyo matokeo yake wanatumbukia katika makatazo matatu: wanakanusha uhakika, kuthibitisha namna kwa kupindisha maana na kumkanushia Mola (Ta´ala) sifa Zake ambazo amejithibitishia Mwenyewe. Kuhusu Wathibitishaji, hakuna yeyote ambaye anapinga chochote ambacho amejithibitishia Allaah (Ta´ala) Mwenyewe.” (Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”, uk. 77)
- Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 140
- Imechapishwa: 17/07/2024
- taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
al-Layth bin Sa´d (afk. <175), mwanachuoni wa Misri.
137 – Mtunzi amesimulia kutoka kwa al-Waliyd bin Muslim, ambaye amesema:
”Nilimuuliza al-Awzaa´iy, al-Layth bin Sa´d, Maalik na ath-Thawriy juu ya Hadiyth zinazozungumzia Kuonekana na nyenginezo. Wakasema: ”Zipitisheni bila ya kuzifanyia namna.”[1]
[1] Imeshatangulia punde kidogo kwa tamko lisemalo:
”Zipitisheni kama zilivyokuja bila ya tafsiri.”
Ibn Taymiyyah amesema:
”Kusema kwamba Hadiyth zipitishwe kama zilivyokuja kuna Radd dhidi ya Wakanushaji. Kusema kwamba zipitishwe bila ya kuzifanyia namna kuna Radd dhidi ya Wafananishaji.” (al-Hamawiyyah)
Ibn-ul-Qayyim amesema:
”Makusudio ya Salaf ”bila ya kuzifanyia namna” ni kukanusha kupindisha maana. Wapindishaji wanadai kupindisha maana, kwa sababu wao ndio wenye kuthibitisha namna inayopingana na uhakika na hivyo matokeo yake wanatumbukia katika makatazo matatu: wanakanusha uhakika, kuthibitisha namna kwa kupindisha maana na kumkanushia Mola (Ta´ala) sifa Zake ambazo amejithibitishia Mwenyewe. Kuhusu Wathibitishaji, hakuna yeyote ambaye anapinga chochote ambacho amejithibitishia Allaah (Ta´ala) Mwenyewe.” (Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”, uk. 77)
Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 140
Imechapishwa: 17/07/2024
taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/117-zipitisheni-kama-zilivyokuja-bila-ya-kuzifanyia-namna/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)