Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
97 – Tunawaamini Malaika, Mitume na Vitabu walivyoteremshiwa Mitume. Tunashuhudia ya kwamba vilikuwa vya haki ilio wazi.
MAELEZO
Haya ni katika nguzo za imani ambazo ya kwanza ni kumuamini Allaah na ya pili ni kuwaamini Malaika. Malaika ni viumbe visivyoonekana ambavyo hakuna awajuaye isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah amewaumba kutokana na nuru ili wamwabudu na watekeleze maamrisho Yake kwa viumbe Wake. Allaah amewapa kazi wanazozisimamia na kuzitekeleza juu ya viumbe Wake. Miongoni mwao wako ambao kazi yao ni Wahy, wengine wamepewa kazi ya kuteremsha mvua na mazao na wengine wamepewa kazi ya kuzitoa roho. Wengine wamepewa kazi ya kupuliza parapanda, wengine wamepewa kazi ya kudhibiti matendo ya wanadamu, wengine wamepewa kazi ya milima, wengine wamepewa kazi ya kuwaangalia watoto ndani ya matumbo ya wajawazito. Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arobaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu. Kisha huwa donge la damu kwa muda kama huo. Kisha huwa pande la nyama kwa muda kama huo. Kisha Allaah humtumia Malaika na akampulizia roho na akaamrishwa aandike maneno manne; riziki yake, muda wake wa kuishi, matendo yake na kama atakuwa mtu muovu au mwema.”[1]
Kwa hivyo wanasimamia kazi walizopewa kama Allaah alivyowaamrisha:
لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ
“Hawamtangulii kwa neno nao kwa amri Yake wanaitekeleza. Anajua yale yaliyoko mbele yao na yale yaliyoko nyuma yao na wala hawamuombei uombezi isipokuwa kwa yule ambaye Amemridhia – nao kutokana na kumkhofu ni wenye kutahadhari. Yeyote yule miongoni mwao atakayesema: “Mimi ni mungu mwabudiwa badala Yake”, basi huyo Tutamlipa [Moto wa] Jahannam. Hivyo ndivyo Tunavyowalipa madhalimu.”[2]
يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ
“Wanasabihi usiku na mchana, wala hawazembei.”[3]
Wanamwabudu Allaah ´ibaadah endelevu na sambamba na hilo wanasimamia zile kazi walizopewa.
[1] al-Bukhaariy (6549) na Muslim (2643).
[2]21:27-29
[3]21:20
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 128-129
- Imechapishwa: 11/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket