Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
96 –Tunaamini kuwa Allaah amemfanya Ibraahiym kuwa kipenzi wa hali ya juu na amemzungumzisha Muusa maneno ya kweli. Tunayaamini hayo, kuyathibitisha na kujisalimisha nayo.
MAELEZO
Miongoni mwa mambo ambayo waislamu wanatakiwa kuamini ni kuwa Mitume ndio viumbe wabora na Mitume wanatofautiana kati yao ubora. Kwa mfano wanaamini ya kwamba Allaah amemfanya Ibraahiym kuwa kipenzi wa hali ya juu:
وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا
“Allaah amemfanya Ibraahiym kuwa ni kipenzi wa karibu.”[1]
Mapenzi ya hali ya juu (خليل) ndio ngazi ya juu kabisa ya mapenzi. Allaah (Jalla wa ´Ala) anawapenda waja Wake waumini na wachaji wafanyao matendo mema, anawapenda waja Wake wenye kutubia na anawapenda waja Wake wenye kujitwahirisha, lakini mapenzi ya hali ya juu hakuna waliyoyapata isipokuwa tu watu wawili: Ibraahiym na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika Allaah amenifanya kuwa kipenzi Wake wa hali ya juu kama alivyomfanya Ibraahiym kuwa kipenzi Wake wa hali ya juu.”[2]
[1]4:125
[2]Muslim (532).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 126-127
- Imechapishwa: 11/11/2024
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
96 –Tunaamini kuwa Allaah amemfanya Ibraahiym kuwa kipenzi wa hali ya juu na amemzungumzisha Muusa maneno ya kweli. Tunayaamini hayo, kuyathibitisha na kujisalimisha nayo.
MAELEZO
Miongoni mwa mambo ambayo waislamu wanatakiwa kuamini ni kuwa Mitume ndio viumbe wabora na Mitume wanatofautiana kati yao ubora. Kwa mfano wanaamini ya kwamba Allaah amemfanya Ibraahiym kuwa kipenzi wa hali ya juu:
وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا
“Allaah amemfanya Ibraahiym kuwa ni kipenzi wa karibu.”[1]
Mapenzi ya hali ya juu (خليل) ndio ngazi ya juu kabisa ya mapenzi. Allaah (Jalla wa ´Ala) anawapenda waja Wake waumini na wachaji wafanyao matendo mema, anawapenda waja Wake wenye kutubia na anawapenda waja Wake wenye kujitwahirisha, lakini mapenzi ya hali ya juu hakuna waliyoyapata isipokuwa tu watu wawili: Ibraahiym na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika Allaah amenifanya kuwa kipenzi Wake wa hali ya juu kama alivyomfanya Ibraahiym kuwa kipenzi Wake wa hali ya juu.”[2]
[1]4:125
[2]Muslim (532).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 126-127
Imechapishwa: 11/11/2024
https://firqatunnajia.com/116-sifa-maalum-kwa-ibraahiym-na-muhammad/