Ni kweli kwamba walikuwepo watu wa upotovu, lakini walikuwa wamenyamaza juu ya upotovu wao. Si lazima jamii yote iwe njema na safi. Hapana budi kuwepo ndani yake watu wa upotovu. Lakini wanapoona nguvu ya haki wananyamaza. Wakipata nafasi, basi huonyesha yale waliyonayo. Ndiyo maana vitabu hivi vilipotafsiriwa kwa kiarabu, shari yao ikaonekana na wakavitumia kama silaha dhidi ya waislamu. Mfano wake ni kama mnavyoona leo, fitina hii iliyokuja kutoka kwa makafiri dhidi ya Uislamu na waislamu. Wakaonekana baadhi ya waislamu wanaowaunga mkono makafiri na kuwaitia watu katika mwito wao. Wakaonekana baadhi ya watoto wa waislamu na wanaojinasibisha na elimu wakijiunga na safu ya makafiri hali ya kuwasaidia, wakiyapenda mawazo yao na wakiyaeneza. Huu ni mwenendo wa Allaah katika viumbe Wake kwamba huwafanyia mitihani waja Wake ili ajulikane muumini wa kweli kutokana na mnafiki:

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَا رَسُولِهِ وَلَا الْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ

”Je, mmedhani kuwa mtaachwa tu na ilihali Allaah bado hajawadhihirisha wale waliopambana jihaad kati yenu na hawakumfanya yeyote kuwa mwandani isipokuwa Allaah na Mtume Wake na waumini wenziwe? Allaah ndiye Mjuzi wa khabari za dhahiri na siri kwa yale mnayoyafanya.”[1]

مَّا كَانَ اللَّـهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ

“Haiwi kwa Allaah kuwaacha waumini katika hali mliyo nayo mpaka ampambanue mbaya na mwema. Na haiwi kwa Allaah akufunulieni ya ghaibu.”[2]

Hatuwajui watu wa shari isipokuwa wakati wa mitihani.

[1] 09:16

[2]3:179

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 184-185
  • Imechapishwa: 07/07/2026