116. Zipitisheni kama zilivyokuja bila ya kuzifasiri

133 – Faqiyh Abu Thawr ameeleza kuwa amemsikia ash-Shaafi´iy akisema:

”Maalik alikuwa akisema pindi anapojiliwa na baadhi ya watu wa matamanio: ”Kuhusu mimi, niko juu ya uwazi wa dini yangu. Kuhusu wewe, ni mwenye mashaka. Hivyo basi, nenda kwa wenye mashaka mfano wako na ugombane naye.”

134 – al-Waliyd bin Muslim amesema:

”Nilimuuliza al-Awzaa´iy, Maalik bin Anas, Sufyaan ath-Thawriy na al-Layth bin Sa´d kuhusu Hadiyth za sifa. Wote wakasema: ”Zipitisheni kama zilivyokuja bila ya tafsiri[1].”[2]

Ameipokea al-Haytham bin Khaarijah kupitia wengi kutoka kwake.

135 – Ibn Abiy Uways amesimulia kuwa amemsikia Maalik akisema:

”Qur-aan ni maneno ya Allaah na maneno ya Allaah yametokea Kwake. Hakuna chochote kinachotokana na Allaah kimeumbwa.”[3]

[1] Bi maana bila ya kuyafanyia namna. Amesema mtunzi baada ya masimulizi hayo:

”Maalik katika zama zake alikuwa ni imamu wa watu wa Madiynah, ath-Thawriy alikuwa ni imamu wa watu wa Kuufah, al-Awzaa´iy alikuwa ni imamu wa watu wa Dameski na al-Layth alikuwa ni imamu wa watu wa Misri. Ni miongoni mwa wanafunzi wakubwa wa wanafunzi wa Maswahabah. Munammad bin al-Hasan – ambaye ni mwanachuoni wa watu wa ´Iraaq – akasimulia maafikiano juu ya jambo hilo.” (al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 82-84)

[2] Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh na wasimulizi wake wote ni madhubuti. Mtunzi ameisahihisha katika “al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn” kupitia kwa al-Haytham. Kupitia kwake ameipokea Ibn Mandah na as-Swaabuuniy katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd” na as-Swaabuuniy katika ”´Aqiydat-us-Salaf wa Asw-hhaab-il-Hadiyth”.

[3] Ameipokea ´Abdullaah katika ”as-Sunnah”, uk. 24-25. Wasimulizi wake ni wenye kuaminika, isipokuwa tu Abu Bakr Ahmad bin Muhammad al-´Umariy, ambaye simtambui.

Ahmad ametaja masimulizi haya, kama alivyopokea Abu Dawuud katika ”Masaa-il-ul-Imaam Ahmad”, uk. 263. Ashaa´irah wamepindisha maana ´Aqiydah hiyo na hivyo wakasema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah kwa maana ya kwamba Ameiumba katika Ubao uliohifadhiwa. Rejea maelezo ya al-Bayjuuriy katika ”al-Jawharah”, uk. 44-45

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 139-140
  • Imechapishwa: 17/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy