116. Vipi Malaika watafunza uchawi ilihali ni kufuru?

Lakini huenda mtu akauliza “Vipi Malaika wanafunza uchawi ilihali kufunza uchawi ni ukafiri?” Haya ni majaribio na mtihani kutoka kwa Allaah. Allaah amewafanya wakafunza uchawi ili kuwapa mtihani watu na kuona ni nani atakayeamini na ni nani atakayekufuru. Malaika hawa wawili wameteremshwa na Allaah wafunze uchawi ili kuwapa mtihani watu na kuona ni nani ambaye ataamini na ni nani atakufuru. Kwa ajili hiyo ndio maana hawamfundishi yeyote katika watu:

وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ

“Na [hao Malaika wawili] hawamfundishi yeyote mpaka wamwambie kwanza: “Hakika sisi ni mtihani, hivyo basi usikufuru [kwa kufanya uchawi].”

Wawili hao wanaanza kumnasihi kwanza yule anayetaka kujifunza kuacha kujifunza uchawi na wanambainishia kuwa ni kufuru. Hawamfunzi yeyote wakakaa kimya. Isipokuwa wanamnasihi na kumbainishia kuwa ni kufuru. Wakiuchagua kwa kutaka kwao wenyewe wanakufuru. Allaah amewaacha Malaika hawa wawili kufunza uchawi ili kuwapa watu mtihani. Haina maana kwamba uchawi hauna ubaya wowote au kwamba unafaa kwa sababu Malaika wanaufunza. Ni kwa ajili ya kuwapa watu majaribio na kuwapa mtihani watu na kuona ni nani atakayeamini na kukufuru, ni nani atakayekubali nasaha na ni nani asiyekubali nasaha. Kutokana na haya tumejua kwamba uchawi ni kufuru. Ni mamoja kule kujifunza nao na kule kuufunza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 149-150
  • Imechapishwa: 31/01/2019