Allaah (Ta´ala) amesema:

عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ

“Adhabu Yangu Nitamsibu nayo yule nimtakaye; na Rahmah Yangu imekienea kila kitu.” 07:156

Imesihi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kutakuwepo watu katika waislamu siku ya Qiyaamah na madhambi mfano wa mlima. Allaah atawasamehe na kuwaweka kwa mayahudi na manaswara.”

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila mmoja ana mahala pake Peponi na Motoni. Muumini anapoingia Peponi kafiri anachukua nafasi yake Motoni kwa kuwa anaustahiki kwa sababu ya ukafiri wake.”

Imekuja katika Hadiyth Swahiyh kwamba utasema:

“Huyu ndiye mwachwa wako nuru kutokamana na Moto.”

Hii ni bishara njema kubwa kwa waislamu wote. ash-Shaafi´iy na ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahumaa Allaah) wamesema Hadiyth hii inawapa waislamu wote matumaini makubwa kwa kuwa inasema wazi kuwa kila muislamu ataachwa huru.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 234
  • Imechapishwa: 25/12/2016