2 – Ndugu yake maiti kumlipia swawm yake ya nadhiri. Kumepokelewa Hadiyth kadhaa juu ya hilo:
1 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyote mwenye kufa na hali anadaiwa swawm, basi walii wake atamfungia nayo.”
Ameipokea al-Bukhaariy (4/156), Muslim (3/155), Abu Daawuud (1/376), kutoka njia yake al-Bayhaqiy (6/279), at-Twahaawiy katika ”Mushkil-ul-Aathaar” (3/140-141) na Ahmad (6/69).
2 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:
”Mwanamke mmoja alipanda baharini ambapo akaweka nadhiri kwamba ikiwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) atamwokoa basi atafunga mwezi mzima. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akamwokoa, hata hivyo hakufunga mpaka akafa. Jamaa yake mmoja [labda dada au msichana wake] akaja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza hayo, akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Je, lau angekuwa na deni ungeweza kulilipa?” Akasema: ”Ndiyo.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Basi deni la Allaah linastahiki zaidi kulipwa.”] Akasema: “Mlipie [kwa niaba ya mama yako.”]
Ameipokea Abu Daawuud (2/81), an-Nasaa’iy (2/143), at-Twahaawiy (3/140), al-Bayhaqiy (4/255-256, 10/85), at-Twayaalisiy (2630), Ahmad (1861, 1970, 3137, 3224, 3420). Tamko ni la Ahmad na ziada ya pili. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim. Ziada ya kwanza ni ya Abu Daawuud na al-Bayhaqiy.
Pia ameipokea al-Bukhaariy (4/158–159), Muslim (3/156), at-Tirmidhiy (2/42–43) ambaye ameisahihisha, na Ibn Maajah (1/535) kwa tamko hilohilo. Wote wameipokea pamoja na ziada ya pili, Muslim peke yake ziada ya mwisho.
3 – Kutoka kwake pia (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:
”Sa´d bin ´Ubaadah (Radhiya Allaahu ´anh) alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akasema: “Hakika mama yangu amefariki na alikuwa na nadhiri.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Lipa kwa niaba yake.”
Ameipokea al-Bukhaariy (5/400, 494), Muslim (6/76), Abu Daawuud (2/81), an-Nasaa’iy (2/130, 144), at-Tirmidhiy (2/375), al-Bayhaqiy (4/256, 6/278, 10/85), at-Twayaalisiy (2717) na Ahmad (1893, 3049, 6/47).
Hadiyth hizi ni za wazi kabisa katika kuthibitisha kukubaliwa katika Shari´ah walii kumfungia maiti swawm ya nadhiri. Hata hivyo Hadiyth ya kwanza inafahamisha kwa ujumla wake kuwa ni zaidi ya hilo, kwani inaonyesha kwamba anafungiwa hata swawm ya faradhi pia. Hayo yamesemwa na Shaafi´iyyah. Vilevile ndio maoni ya Ibn Hazm (7/2-8) na wengineo. Hanaabilah wameonelea maoni ya kwanza. Bali ni tamko la wazi la Imaam Ahmad, ambapo Abu Daawuud amesema katika ”al-Masaa-il” (96):
“Nimemsikia Ahmad bin Hanbal akisema: ”Maiti hafungiwi isipokuwa katika nadhiri tu.”
Wafuasi wake wamebeba maana ya Hadiyth ya kwanza juu ya swawm ya nadhiri, kwa dalili ya yale yaliyopokewa kutoka kwa ´Amrah kwamba mama yake alikufa na alikuwa anadaiwa siku za Ramadhaan. Akaenda kwa ´Aaishah na akamuuliza: “Je, nifunge kwa niaba yake?” Akamjibu: ”Hapana, bali mtolee swadaqah kwa kila siku nusu pishi juu ya masikini mmoja.”
Ameipoikea at-Twahaawiy (3/142) na Ibn Hazm (7/4) ambaye tamko ni lake kwa cheni ambayo Ibn at-Turkumaaniy amesema: ”Swahiyh.” Hata hivyo imedhoofishwa na al-Bayhaqiy na al-´Asqalaaniy. Ikiwa wameidhoofisha kwa sababu ya cheni hii, basi hawakuwa na hoja, na ikiwa walikusudia njia nyingine, basi hilo halidhuru. Kuna dalili nyingine pia kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:
“Mtu akiumwa katika Ramadhaan kisha akafa na hakufunga, basi atatolewa fidia kwa niaba yake. Lakini ikiwa alikuwa na nadhiri, basi walii wake atamlipia nayo.”
Ameipokea Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kwa masharti al-Bukhaariy na Muslim. Aidha inayo njia nyingine kama hiyo kwa Ibn Hazm (7/7) ambaye pia amesahihisha cheni yake ya wapokezi. Vilevile inayo njia ya tatu kwa at-Twahaawiy (3/142), lakini inaonekana kuwa kuna sehemu ya matini imeondoka ama na mnakshi au mchapa nakala, hivyo maana yake ikaharibika.
Ufananuzi huu ambao ameona mama wa waumini; ´Aaishah na mfasiri mkubwa wa ummah ambaye ni Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na wakafuatwa na Imaam wa Sunnah; Ahmad bin Hanbal ndio mtazamo ambao moyo unatulizana nao na kifua kinafunguka kwa ajili yake. Huu ndio mtazamo wa kati kati na wa haki zaidi katika suala hili. Jengine ni kwamba unakusanya Hadiyth zote bila kuzipinga yoyote kati yao, pamoja na uelewa sahihi na khaswa Hadiyth ya kwanza. Hili halikueleweka kwa mama wa waumini kama maana ya jumla ya kufunga Ramadhaan kwa niaba ya maiti, isitoshe yeye ndiye msimulizi wa Hadiyth hiyo. Isitoshe miongoni mwa mambo yaliyothibitishwa ni kwamba msimulizi wa Hadiyth anajua zaidi maana ya kile alichopokea, khaswa pale ambapo alichoelewa kinaenda sambamba na misingi ya Shari´ah na kanuni zake, kama ilivyo hapa. Hilo limebainishwa na mkaguzi Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) katika “I´laam-ul-Muwaqqy´iyn” (3/554) aliposema baada ya kunukuu Hadiyth hiyo na kuisahihisha:
“Kundi moja limeichukua Hadiyth hiyo kwa ueneaji na kuachiwa kwake na kusema kwamba maiti anafungiwa swawm ya nadhiri na ya faradhi. Kundi jingine likapinga kabisa na kusema kwamba anafungiwa swawm ya nadhiri tu bila ya swawm ambayo msingi wake ni faradhi. Haya ya pili ndio maoni ya Ibn ´Abbaas na wanafunzi wake, nayo ndio sahihi. Kwa sababu faradhi ya swawm ni kama swalah; kama ambavyo hakuna anayeswali kwa niaba ya mwingine wala salamu haitolewi kwa niaba ya mwingine, basi ndivyo hivyo pia inapokuja katika swawm. Ama nadhiri ni jambo lililobebwa na dhamira kama deni, basi inakubalika kulipwa na walii kama vile linalovyolipwa deni lake. Huo ndio uelewa halisi.
Kwa muktadha huu ni kwamba haifai kuhiji kwa niaba yake wala kutoa zakaah kwa niaba yake isipokuwa kama alikuwa na udhuru wa kuchelewesha, kama vile inavyoruhusiwa kwa walii kutoa fidia ya kula kwa niaba ya aliyekula katika Ramadhaan kwa udhuru. Ama aliyeacha kufunga bila udhuru wowote, basi hakuna faida yoyote mtu mwingine kumfanyia matendo ya faradhi za Allaah ambazo alizembea kuzifanya, kwani yeye ndiye aliyekuwa ameamrishwa nazo kwa ajili ya mtihani na majaribio, siyo walii wake. Hivyo haitamnufaisha tawbah ya mtu mwingine, Uislamu wa mtu mwingine kwa niaba yake, swalah ya mtu mwingine kwa niaba yake wala matendo mengine yoyote kati ya faradhi za Allaah ambazo alizembea mpaka akafa.”
Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ameongeza ufafanuzi na uchambuzi zaidi wa masuala haya katika “Tahdhiyb-us-Sunan” (3/279–282). Hivyo mtu arejee huko kwani ni muhimu.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 213-216
- Imechapishwa: 02/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 213-216
Imechapishwa: 02/08/2026
https://firqatunnajia.com/113-maiti-ananufaika-kwa-ndugu-yake-kumlipia-swawm-ya-nadhiri/