Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

93 – Hata hivyo haihitajii ´Arshi na vyenginevyo.

MAELEZO

Usifikiri maneno Yake (Ta´ala):

ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ ٌ

”… kisha Akalingana juu ya ´Arshi.”[1]

kuwa ni mwenye kuhitajia ´Arshi hiyo kama ambavyo kiumbe analingana juu ya kiumbe kingine. Allaah (´Azza wa Jall) amelingana juu ya ´Arshi na wakati huohuo si mwenye kuihitajia wala kitu kingine. Lakini viumbe wote ni wenye kumuhitajia Yeye:

إِنَّ اللَّـهَ يُمْسِكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ أَن تَزُولَا ۚ وَلَئِن زَالَتَا إِنْ أَمْسَكَهُمَا مِنْ أَحَدٍ مِّن بَعْدِهِ

“Hakika Allaah anazuia mbingu na ardhi zisiondoke na zikiondoka basi hakuna yeyote wa kuzishikilia baada Yake.”[2]

Yeye ndiye ambaye anazuia´Arshi, mbingu, ardhi na viumbe vyengine vyote kwa uwezo na nguvu Zake. Wao ndio wenye kumuhitajia, lakini Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) hawahitajii. Kwa sababu kitu kiko juu ya kingine, haina maana kwamba kile kilicho juu kinahitaji kilichoko chini yake. Mbingu ziko juu ya ardhi lakini hazihitaji ardhi.

[1]57:4

[2]35:41

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 125-126
  • Imechapishwa: 10/11/2024