Swali: Mwanamme ana wake wawili na mke mmoja ana matangamano mazuri kwa mume wake kuliko yule mwingine inapokuja katika chakula, mavazi na malazi. Je, inafaa kwake kumfadhilisha juu ya yule mwingine?
Jibu: Ni lazima kwake kufanya uadilifu kati ya wake zake wawili. Allaah (Subhaanah) ameusia kufanya uadilifu. Ni lazima kwake kufanya uadilifu na ni lazima kwake vilevile kumfunza yule ambaye maadili yake yamekuwa mabaya au anafanya upungufu juu ya haki yake. Ni lazima kwake kumfunza na kumwelekeza katika kheri kwa hekima na maneno mazuri. Imesihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:
“Yule ambaye atakuwa na wake wawili ambapo akampendelea mmoja wao, basi atakuja siku ya Qiyaamah na ubavu wake mmoja umepinda.”
Yale mambo ambayo ana uwezo juu yake kugawanya kati yao katika wakati, hali zake zote na matumizi. Kuhusu yale ambayo hayamiliki upande wa mapenzi na yanayofuatia katika jimaa si mambo ambayo yanamlazimu kufnaya uadilifu. Mapenzi yako mikononi mwa Allaah na hayako mikononi mwake yeye. Mmoja anaweza kuwa ni mwenye kupendwa zaidi kuliko mwingine na anaweza kuwa anamtamani zaidi mmoja kuliko mwingine. Sio kwa khiyari yake. Hapa halazimiki kufanya uadilifu. Wala hapati dhambi akimjamii mmoja zaidi anavomjamii mwingine au akampenda mmoja zaidi kuliko anavompenda mwingine. Kwa sababu jambo hilo liko mikononi mwa Allaah na haliko mikononi mwa mja.
Lakini kufanya uadilifu kwa kumpa haki yake ya mchana wake, usiku wake na matumizi yake ni mambo ya lazima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Wana juu yenu riziki zao na mavazi yao kwa wema.”
Hakusema kufanya uadilifu kati yao katika jimaa au katika mapenzi. Hayo ni mambo asiyoyamiliki mtu. Hayako katika khiyari yake.
Lakini ikiwa mmoja wao anatangamana naye vibaya na hamtekelezei yaliyo ya wajibu, basi amfundishe, amwelekeze na atangamane naye yale yanayolazima katika kutengeneza kama vile mawaidha, kukumbusha, kususa na kuadabisha haja ikipelekea kufanya hivo baada ya kutonufaisha kukata na mawaidha.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4304/حكم-تفضيل-احدى-الزوجتين-لتقصير-الاخرى
- Imechapishwa: 15/06/2022

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4304/حكم-تفضيل-احدى-الزوجتين-لتقصير-الاخرى
Imechapishwa: 15/06/2022
https://firqatunnajia.com/112001-2/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)