3 – Jundub bin ´Abdillaah al-Bajaliy amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku tano kabla ya kufa akisema:

”Zindukeni! Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Mitume na waja wao wema kuwa ni mahali pa kuswalia. Zindukeni! Msiyafanye makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia. Hakika mimi nakukatazeni na jambo hilo.”[1]

[1] Muslim (532), Abu ´Awaanah na Ibn Sa´d. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa wale waliokuwa kabla yenu waliyafanya makaburi ya Mitume na waja wao wema kuwa ni mahali pa kuswalia. Kisha akayawekea maelezo wasifu wao kwa makatazo. Kwa msemo mwingine haifai wakayafanya makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametukataza kutokana na jambo hilo. Hilo linafahamisha kwa njia moja au nyingine kuwa tumekatazwa kulifanya hilo kwa sababu lilifanywa na wale waliokuwa kabla yenu. Hilo linapelekea kuwa matendo yao ima ni dalili na alama ya kwamba Allaah ametukataza kufanya hayo au pia ni sababu inayopelekea katika makatazo hayo. Kwa hali yoyote ile, ni jambo linatakikana katika Shari´ah kule kwenda kinyume nao. Makatazo ya kitendo hichi kwa kulaaniwa mayahudi na manaswara ni jambo limepokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… Hapa si wakati na mahala pake kuzitaja dalili zote hizo, kwa sababu lengo ni ile kanuni yenye kuenea. Vilevile wanazuoni wa madhehebu mengi, wakiwemo wafuasi wa Maalik, ash-Shaafi´iy na Ahmad, wametaja uharamu wa jambo hilo.” (Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 52)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 171-172
  • Imechapishwa: 01/11/2023