112. Hata kama watu wote watakukana

Ibn Jurayj (afk. 150), Shaykh wa Haram na Muftiy wa Hijaaz.

120 – Abu Haatim ar-Raaziy amesimulia kutoka kwa al-Answaariy, kutoka kwa Ibn Jurayj (Rahimahu Allaah), ambaye amesema:

”´Arshi Yake ilikuwa juu ya maji kabla ya kuwaumba viumbe.”

Abu ´Amr ´Abdur-Rahmaan bin ´Amr al-Awzaa´iy (afk. 157), mwanachuoni wa watu wa Shaam katika zama zake.

121 – Abu ´Abdullaah al-Haakim amepokea kwamba al-Awzaa´iy amesema:

”Tulikuwa wakati ambao wanafunzi wa Maswahabah wamejaa: ”Hakika Allaah (Ta´ala) Yuko juu ya ´Arshi Yake na tunaziamini zile sifa Zake zilizopokelewa na Sunnah.”[1]

Ameipokea al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa´ was-Swifaat”.

122 – Mfasiri wa Qur-aan Abu Ishaaq ath-Tha´labiy amepokea:

”al-Awzaa´iy aliulizwa kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

”thuma stawa…arshi” 7:54

Akajibu: ”Yuko juu ya ´Arshi Yake kama Alivyojisifia Mwenyewe.”

123 – al-Waliyd bin Muslim alimuuliza Imaam Abu ´Amr al-Awzaa´iy kuhusu Hadiyth zinazozungumzia sifa, ambapo akajibu:

”Zipitisheni kama zilivyokuja.”

Miongoni mwa masimulizi ya Imaam huyu ni pamoja na:

“Lazimiana na masimulizi ya waliotangulia hata kama watu watakukataa. Na jihadhari na maoni ya watu hata kama watakupambia nayo kwa maneno.”[2]

[1] Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Taymiyyah katika ”at-Tadmuriyyah”, na Ibn-ul-Qayyim akaafikiana naye katika “Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”, uk. 43.  Mtunzi amesema katika ufupisho wake kwamba ”Wapokezi wake ni maimamu na wenye kuaminika”.

[2] Ameipokea al-Ajurriy katika ”ash-Shariy´ah”, uk. 102, kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 137
  • Imechapishwa: 14/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy