110. Sijui kama Allaah yuko juu ya mbingu au ardhini

118 – Tumefikiwa na khabari kwamba Abu Mutwiy´ al-Hakam bin ´Abdillaah al-Balkhiy[1], bwana wa ”al-Fiqh al-Akbar”, aliyesema:

”Nilimuuliza Abu Haniyfah juu ya mwenye kusema kwamba yeye hajui kama Mola yuko juu juu ya mbingu au ardhini. Akasema: ”Amekufuru, kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[2]

´Arshi Yake iko juu ya mbingu Zake.”  Nikasema kuwa bwana huyo anasema kuwa Amelingana juu ya ´Arshi, lakini eti hajui kama ´Arshi iko juu ya mbingu au ardhini.” Akasema: ”Akipinga kwamba Yuko juu ya mbingu basi amekufuru.”[3]

Ameipokea mtunzi wa ”al-Faaruuq”.

[1] Abu Mutwiy´ huyu ni katika maswahiba wakubwa wa Abu Haniyfah na wanazuoni wao. Mtunzi amesema:

”Alikuwa ni mwenye uoni wa ndani, mwenye elimu iliobobea na mwenye nafasi ya juu. Lakini alikuwa ni dhaifu mno inapokuja katika kudhibiti masimulizi. Ibn-ul-Mubaarak alikuwa akimuadhimisha na akimtukuza inapokuja katika dini na elimu yake, ilihali Ibn Ma´iyn amesema kuwa yeye si chochote.” (Miyzaan-ul-I´tidaal)

[2] 20:05

[3] Katika maneno ya mtunzi ”bwana wa ”al-Fiqh al-Akbar” kuna ishara yenye nguvu kwamba kitabu ”al-Fiqh al-Akbar” hakikuandikwa na Imaam Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah), tofauti na vile wanavoona Hanafiyyah. Wamechapisha chapa nyingi wakizinasibisha kwake na zikitolewa maelezo na Hanafiyyah wengi, akiwemo Abu Mansuur al-Maaturiydiy ambaye ´Aqiydah yake inafuatwa na Hanafiyyah wengi. Wengi wao ni katika Mu´awwilah. Utaona namna ambavyo Abu Mansuur huyu alivyokengeusha maneno ya Abu Haniyfah katika ”al-Fiqh al-Akbar” makengeusho kiasi cha kwamba anafikia kuharibu tafsiri ya maneno ya Abu Haniyfah na kumtoa nje ya Salaf ambao hawapindishi maana. Amesema wakati alipokuwa akifasiri maneno yake (Rahimahu Allaah) ”Amekufuru”:

”Kwa sababu anayesema hivo anatoa hisia kwamba Yuko katika mahali fulani na hivyo anakuwa ni mshirikina.”

Hakujali kabisa kujali maneno yake yaliyobakia yanayobatilisha tafsiri yake, nayo ni:

”… kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”

Hii ni dalili ya wazi inayoonyesha kuwa sababu ya kukufuru ni kule kupinga kwake yale yanayofahamishwa waziwazi na Aayah kuhusiana na kuwa Kwake Allaah (Subhaanah) juu ya ´Arshi, na si kwamba anatoa hisia kwamba Yuko mahali fulani. Allaah ametakasika kutokana na hilo! Ibn Abiyl-´Izz al-Hanafiy amesema:

”Usiwajali wale wanaoyapinga hayo ambao wanajinasibisha na madhehebu ya Abu Haniyfah. Mapote mengi, wakiwemo Mu´tazilah, wamejinasibisha naye. Hata hivyo wanapingana naye katika mambo mengi ya ´Aqiydah. Ni kama ambavo wako watu wengi ambao wanajinasibisha na Maalik, ash-Shaafi´iy na Ahmad na wakati huohuo wanapingana nao katika mambo mengi ya ´Aqiydah. Kisa cha Abu Yuusuf ambacho alimtaka Bishr al-Mariysiy kutubia kwa sababu ya kupinga kwake Allaah kuwa juu ya ´Arshi kinajulikana na kimepokea Ibn Abiy Haatim na wengineo.” (Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 323)

Kisa hicho kinachoashiriwa kinakuja karibuni wakati wa masimulizi ya Abu Yuusuf. Kinajulisha kuwa wafuasi wa Abu Haniyfah wa mwanzo walikuwa na ´Aqiydah hiyohiyo kama Salaf juu ya kuamini kuwa juu kwa Allaah (Ta´ala) juu ya viumbe Wake. Ni jambo linaloyatia mapokezi haya nguvu fulani yaliyopokelewa kutoka kwa Abu Haniyfah. Mmoja wao ni Imaam Abu Ja´far at-Twahaawiy al-Hanafiy:

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 136
  • Imechapishwa: 14/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy