Inampasa mwalimu awe mpole kwa anayesoma kwake, amkaribishe na amfanyie wema kwa kadiri ya hali yake. Tumesimuliwa kutoka kwa Abu Haaruun al-´Abdiy, ambaye amesema:
”Tulikuwa tunamwendea Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye husema: ”Karibuni, enyi wasia wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)! Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema: ”Hakika watu ni wenye kukufuateni nyinyi. Hakika wanaume watakuja kwenu kutoka pembe mbalimbali za dunia wakijifunza dini. Kwa hivyo wanapokujieni basi wapokeeni kwa wema.”[1]
Tumesimuliwa mfano wa hayo katika ”al-Musnad” ya ad-Daarimiy kupitia kwa Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh).
[1] at-Tirmidhiy (2650), aliyesema kuwa Shu´bah amemdhoofisha Abu Haaruun al-´Abdiy. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2650).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 29
- Imechapishwa: 19/08/2026
Inampasa mwalimu awe mpole kwa anayesoma kwake, amkaribishe na amfanyie wema kwa kadiri ya hali yake. Tumesimuliwa kutoka kwa Abu Haaruun al-´Abdiy, ambaye amesema:
”Tulikuwa tunamwendea Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye husema: ”Karibuni, enyi wasia wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)! Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema: ”Hakika watu ni wenye kukufuateni nyinyi. Hakika wanaume watakuja kwenu kutoka pembe mbalimbali za dunia wakijifunza dini. Kwa hivyo wanapokujieni basi wapokeeni kwa wema.”[1]
Tumesimuliwa mfano wa hayo katika ”al-Musnad” ya ad-Daarimiy kupitia kwa Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh).
[1] at-Tirmidhiy (2650), aliyesema kuwa Shu´bah amemdhoofisha Abu Haaruun al-´Abdiy. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2650).
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 29
Imechapishwa: 19/08/2026
https://firqatunnajia.com/11-upole-wa-mwalimu/