Imaam Muwaffaq-ud-Diyn amesema:

”Nimefikiwa na khabari kwamba Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) amesema katika ”al-Fiqh al-Akbar”:

”Mwenye kupinga ya kwamba Allaah (Ta´ala) yuko juu ya mbingu amekufuru.”[1]

 Maalik amesema:

”Allaah yuko juu ya mbingu na utambuzi Wake uko kila mahali.”[2]

Ameipokea ´Abdullaah bin Ahmad katika “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”.

Amesema tena:

”Kulingana Kwake juu si kwamba hakufahamiki. Namna haifahamiki. Ni wajibu kuamini hilo na kuulizia hilo ni Bid´ah.”[3]

Haya yamesihi na kuthibiti kutoka kwa Maalik. Ameipokea al-Bayhaqiy na wengineo.

Muqaatil bin Hayyaan amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا

“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala chini kuliko ya hivyo na wala wengi zaidi isipokuwa Yeye yupamoja nao popote watakapokuwa, kisha siku ya Qiyaamah atawajulisha yale waliyoyatenda; hakika Allaah juu ya kila jambo ni mjuzi.”[4]

“Yuko (Ta´ala) juu ya ´Arshi na utambuzi Wake uko pamoja nao.”

Ameipokea ´Abdullaah bin Imaam Ahmad bin Hanbal.

Sulaymaan bin Harb amesimulia kuwa amemsikia Hammaad bin Zayd akisema:

”Hakika si vyengine ni kwamba wanazungukia kusema kuwa hakuna mungu juu ya mbingu.”

Ameipokea  Ibn Abiy Haatim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Sulaymaan bin Harb.

´Aliy bin al-Hasan bin Shaqiyq amesema:

”Nilimuuliza ´Abdullaah bin al-Mubaarak: ”Ni vipi tutamtambua Mola wetu (´Azza wa Jall)?” Akasema: ”Kwamba Yuko juu ya mbingu ya saba, juu ya ´Arshi Yake. Hatusemi kama wanavosema Jahmiyyah, kwamba Yuko hapa ardhini.”

Ameipokea ´Abdullaah bin Ahmad, kutoka kwa Ahmad bin Ibraahiym ad-Dawraqiy, kutoka kwa ´Aliy.

´Abdullaah amepokea tena:

”Bwana mmoja alimwambia Ibn-ul-Mubaarak: ”Ee Abu ´Abdir-Rahmaan! Nimekuwa ni mwenye kuogopa mbele ya Allaah (´Azza wa Jall) kutokana na wingi wa du´aa nilizoziomba dhidi ya Jahmiyyah.” Akasema: ”Usiogope. Kwani hakika wao wanadai kuwa Mola wako ambaye yuko juu ya mbingu si chochote.”

Jariyr bin ´Abdil-Hamiyd amesema:

”Maneno ya Jahmiyyah mwanzo wake ni asali na mwisho wake ni sumu. Wanachojaribu ni wao kusema kwamba juu ya mbingu hakuna mungu yeyote.”

Ameipokea Ibn Abiy Haatim.

[1] Ithbaat Swifat-il-´Uluww, uk. 116-117.

[2] at-Tamhiyd (7/138).

[3] al-Asmaa’ was-Swifaat (2/305-306).

[4] 58:7

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 50-53
  • Imechapishwa: 21/12/2025