11. Mume kumuosha mke wake na msichana mdogo

Swali 11: Je, inasihi kwa mwanamme kumuosha mke wake anapokufa au msichana wa miaka mwaka mmoja au miwili ingawa atakuwa ni wa kando kwake[1]?

Jibu: Hapana vibaya mwanamme kumuosha mke wake na mwanamke mume wake. Kwa sababu hilo limetajwa katika Sunnah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutoka kwa Salaf. Ama mbali kumuosha mwengine asiyekuwa mke – kama mama au msichana – haijuzu kwa mwanamme kuwaosha wala wengine wasiokuwa wao katika wale Mahaarim zake wa kike. Anaambatanishwa na mke kijakazi ambaye imehalalika kwake kumjamii. Hapana neno kumuosha akifa kwa sababu yeye pia ni kama mke. Vivyo hivyo msichana mdogo ambaye yuko chini ya miaka saba hapana vibaya kwa mwanamme kumuosha. Ni mamoja ni Mahram wake au wa kando kwake. Kwa sababu hana uchi unaoheshimika. Vivyo hivyo inafaa kwa mwanamke kumuosha mtoto wa kiume ambaye yuko chini ya miaka saba.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/108-109).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 12/12/2021