12. Mafungamano ya kindoa hayamalizika kwa kifo

Swali 12: Nimewasikia wengi wasiokuwa na elimu wakisema kwamba mke anaharamika kwa mume wake baada ya kufa kwake na kwamba haijuzu kumwangalia wala kumweka kwenye mwanandani kaburi lake. Je, haya ni sahihi[1]?

Jibu: Dalili za ki-Shari´ah zimejulisha ya kwamba hapana vibaya kwa mke kumuosha mume wake na kumwangalia. Aidha hapana vibaya kwake mume kumuosha na kumwangalia. Asmaa´ bint ´Umays (Radhiya Allaahu ´anhaa) alimuosha mume wake Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh). Vilevile Faatwimah aliacha anausia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ndiye amuoshe.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/109-110).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 18
  • Imechapishwa: 12/12/2021